Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Peresi (katikakti) akifungua jana mafunzo ya siku 10 ya Wadadisi wa sensa ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa mikoa ya Tabora , Katavi, Shinyanga, Singida na Kigoma ikiwa ni sehemu ya kuwaandaa kwenda kukusanya taarifa za sekta hizo itakayoanza Mwezi ujao hadi Septemba.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Peresi (katikakti) akiwaongoza viongozi na washiriki wa mafunzo ya siku 10 ya Wadadisi wa sensa ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa mikoa ya Tabora , Katavi, Shinyanga, Singida na Kigoma ikiwa ni sehemu ya wakiwa kimya kwa dakika moja kwa ajili ya kumuombea Hayati Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa.
Kaimu Katibu Tawala Mussa Hussein akitoa salamu za Mkoa jana wakati .mafunzo ya siku 10 ya Wadadisi wa sensa ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa mikoa ya Tabora , Katavi, Shinyanga, Singida na Kigoma ikiwa ni sehemu ya kuwaandaa kwenda kukusanya taarifa za sekta hizo itakayoanza Mwezi ujao hadi Septemba.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Peresi (katikakti) akiwa katika picha ya pamoja jana na baadhi ya washiriki wa jana mafunzo ya siku 10 ya Wadadisi wa sensa ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa mikoa ya Tabora , Katavi, Shinyanga, Singida na Kigoma ikiwa ni sehemu ya kuwaandaa kwenda kukusanya taarifa za sekta hizo itakayoanza Mwezi ujao hadi Septemba.
……………………………………………………………………………
WADADISI wa Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa kilimo 2019/20 wametakiwa kuhakikisha takwimu watakazotoa ziwe kweli ili kuiwezesha Serikali kupanga Sera, mipango mbalimbali ya kuwaendeleza, kuimarisha kiuchumi na kuboresha hali ya maisha ya wananchi.
Kauli hiyo imetolewa jana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Peres Magiri wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Wadadisi wa Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa kilimo kwa mikoa ya Tabora, Shinyanga, Kigoma, Katavi na Singida.
Alisema sensa hiyo ni muhimu kwa kuwa ina lengo la kufahamu hali halisi ya kilimo, ufugaji na shughuli za uvuvi kwa kuwa na takwimu zitakazoonesha hali halisi ya sekta hizo nchini ambazo zitatumika kufuatilia viashiria vya Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Mwaka 2030.
Magiri alisema ni muhimu katika kuwa na mipango ambayo itasaidia katika kutokomeza njaa kwa kuwa na uhakika wa chakula kuptia ukuzaji wa kukuza Kilimo.
Aliwataka wananchi hadi viongozi katika mikoa yote kuipa uzito Sensa hii kwa kuhakikisha inafanyika kwa ufanisi ili itoe matokeo tarajiwa.
Magiri alisema kilimo ni muhimu katika uchumi na maendeleo ya nchi ambapo kwa mwaka 2019, kilimo kilichangia katika Pato la Taifa kwa asilimia 26.6 na kwa upande wa mauzo ya nje asilimia 24.3 ya fedha za kigeni zilizopatikana zilitokana na mazao ya kilimo.
Aidha Kaimu Mkuu huyo Mkoa aliwataka Wadadisi kuhakikisha watumia mbinu walizofundishwa na nyingine za ubunifu kupata takwimu sahihi hasa kwenye jamii za wafugaji ambao mara nyingine hawapendi kutaja idadi halisi ya mifugo yao.
sekta ya kilimo kujivunia mchango wetu huu kwa sababu tumechangia na tunaendelea kuchangia katika maendeleo tunayoyaona hivi sasa.
Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Philemon Mwenda aliwataka Wadadisi kufanyakazi kwa bidii na maarifa na hususani jinsi kutumia ya Vishikwambi katika kukusanya takwimu husika.
Alisema kuwa kutakuwepo na usimamizi wa karibu na kama itabainika mdadisi yoyote anakakiuka maadili ya ukusanyaji wa takwimu hizo kwa wakuu wa kaya Sheria hii itachukua mkondo wake ipasavyo.
Kwa upande wa Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Mussa Hussein alisema ni vema Wadadisi waliopewa jukumu hilo za kukusanya takwimu katika ngazi ya Halmashauri kuhakikisha zinakuwa halisi na sio za kutengeneza.