Home Mchanganyiko KIFO CHA MKAPA KIMENIUMIZA SANA –MWANA FA

KIFO CHA MKAPA KIMENIUMIZA SANA –MWANA FA

0


MSANII
wa muziki wa Bongo Fleva nchini Hamisi Mwinyuma alimaarufu Mwana FA
amesema kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa
kimemuumiza na ni pigo kubwa kwa wasanii kutokana na mchango wake wa
kuanzisha Cosota.

Mwana FA aliyasema hayo leo wakati akizungumza
katika wa ibada maalumu ya maombolezo iliyofanyika wilayani Muheza
kwenye viwanja wa Jitegemee na kuongozwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza
Mhandisi Mwanasha Tumbo  na wananchi wakiwemo viongozi wa dini.

Alisema
kutokana na msiba huo mzito ndio maana akaamua kuungana na wananchi wa
wilaya ya Muheza katika halfa hiyo kwa sababu katika kipindi chake ndio
miongoni mwa taasisi aliyonzisha katika kusimamia haki za wasanii. 

Msanii
huyo alisema Cosota ni taasisi inayoshughuli na haki miliki za wasanii
tokea ilipoanzishwa 1996 na imekuwa na mchango mkubwa kwani kabla ya
hapo kazi za wasanii zilikuwa huwezi kumpeleeka mtu mahakamani.


Hata
hivyo alisema kutokana na hilo wana mshukuru Hayati Mkapa kutokana na
mambo makubwa aliyowafanyia wasanii hapa nchini ambayo yamekuwa na tija
kubwa kwao .