Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Bw.Aggrey Mlimkua akizungumza na wadau mbalimbali walioweza kuhudhulia mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wadau mbalimbali walioweza kuhudhulia mkutano huo leo jijini Dar es Salaam
NA EMMANUEL MBATILO
Serikali kupitia maabara ya kuboresha mazingira ya kibiashara na uwekezaji nchini kwa mwaka 2014 waajiriwa wenye kiwango stahiki cha ujuzi nchini ni asilimia 17.
Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Ajira, Bunge na uwekezaji, Doroth Mwaluko wakati wa mkutano wa 60 wa mwaka wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE).
Mh.Doroth amesema kuwa kutokana na kiwango hicho wakadhamilia mpaka ifikapo 2018 angalau kiwango kiwe kimeongezeka na kufikia asilimia 46 ya Waaajiri wenye kiwa hicho.
“Kupitia kuboresha mazingira ya kibiashara tumeona namna ambavyo asilimia imeongezeka ya wenye ujuzi stahiki”amesema Mh.Doroth.
Naye amesema kila mwaka wamekuwa wakifanya mkutano mkubwa na kukutana na wadau mbalimbali ili kuona ni namna gani wanaboresha masuala ya ajiri na kuondoa changamoto zilizopo.
Aidha Bw.Mlimuka amesema changamoto kubwa ambayo imekuwa ikiwakabili ni vijana wengi kukosa ujuzi na uzoefu wa masuala mbalimbali.
Hata hivyo Bw. Mlimuka amesema ndiyo maana wamewataka waajiri kuwapa nafasi vijana waliotoka shule ili kuongeza uzoefu wao.
“Kupitia uzoefu ambao watapata itawasaidia vijana wengi kuwa na ujuzi wa kufanya kazi mahala popote”amesema Bw. Mlimuka.
Pia aliongeza kupitia ujuzi watakaoupata vijana basi kutahirahisishia nchini kufikia kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.