Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),Titus Kaguo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma kuhusu hali ya upatikanaji wa nishati ya mafuta nchini.
……………………………………………………………………………………
Na. Alex Sonna, Dodoma
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA) imetoa onyo kali kwa wauzaji wa mafuta nchini kutoficha mafuta hasa kipindi hiki cha kuelekea kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),Titus Kaguo,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya upatikanaji wa nishati ya mafuta nchini.
Kaguo amesema kuwa kuna baadhi ya vituo vya kuuza vinapakuwa na mafuta kwenye matenki na kuweka kwenye madumu na kuuza kwa walanguzi kitu ambacho kinakiuka kanuni, taratibu na sheria za mafuta.
Lakini pia Kaguo ametoa mwezi mmoja kwa wenye vituo vya mafuta kuwa na mkataba wa kununua mafuta kwa wauzaji wakubwa ili kuimarisha hali ya mafuta nchini katika kuelekea kampeni za uchaguzi mkuu.
“Hivyo ni vyema wafanya biasha kuheshimu kanuni na taratibu za biashara ya nishati ya mafuta ili kutoa ushirikiano kwa serikali yenu katika kuwatumikia watanzania”, amesisitiza Kaguo