Bw. Bernald Kamilius Membe akizungumza na waandishi wa habari leo kabla ya kukabidhiwa fomu za kuomba kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo.
Bw. Bernald Kamilius Membe akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhiwa fomu za kuomba kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo.
Katibu Mkuu wa chama hicho Ado Shaibu akizungumza kabla ya kumkabidhi fomu za kuomba kugombea urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo Bw. Bernald Kamilius Membe leo.
…………………………………………..
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, leo Julai 17, 2020 amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT-Wazalendo ambapo amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu Mkuu wa chama hicho Ado Shaibu.
Membe amesema kuwa leo ametekeleza uwajibu huo kwa maandishi ana furaha baada ya kukabidhiwa fomu hiyo.
“Leo sitakuwa na mengi ya kuongea siku nitakapo rejesha fomu nitamwaga cheche”
Waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje, alifukuzwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tarehe 28 Februari 2020 na Kamati Kuu ya chama hicho, kisha uamuzi huo kubarikiwa na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), tarehe 10 Julai 2020.
Membe alifukuzwa kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya CCM, pamoja na kuonywa mara kadhaa, pasina kubadilika.Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, leo Julai 17, 2020 amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT-Wazalendo ambapo amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu Mkuu wa chama hicho Ado Shaibu.
Membe amesema kuwa leo ametekeleza uwajibu huo kwa maandishi ana furaha baada ya kukabidhiwa fomu hiyo.
“Leo sitakuwa na mengi ya kuongea siku nitakapo rejesha fomu nitamwaga cheche”
Waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje, alifukuzwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tarehe 28 Februari 2020 na Kamati Kuu ya chama hicho, kisha uamuzi huo kubarikiwa na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), tarehe 10 Julai 2020.
Membe alifukuzwa kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya CCM, pamoja na kuonywa mara kadhaa, pasina kubadilika.