…………………………………………………………….
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Mpwapwa.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma, Mh. Jabir Shekimweri, amewaagiza wataalamu wa mifumo ya teknolojia hapa nchini kuangalia uwezekano wa kuitumia mifumo hiyo kwa kutoa elimu ya namna ya kudhibiti malaria hasa katika maeneo ya vijijini.
Mh. Shekimweri amesema kwa nyakati hizi, simu za mikononi zenye mitandao ya kijamii zimeenea kila mahala, hivyo ikiwepo namna nzuri ya kufikusha ujumbe utakaosaidia wananchi kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguuka, kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza mazalia ya mbu wanaosababisha maambukizi ya Malaria.
Alikua azindua mpango wa matumizi salama ya vyandarua vyenye dawa vilivyotolewa na Serikali kwa lengo la kutokomeza malaria hapa nchini mafunzo yaliyofanyika mjini Mpwapwa.
Mafunzo hayo yamewashirikisha wataalamu mbalimbaalia kutoka wilaya za Kongwa na Mpwapwa mkoani Dodoma wakiwemo Wakuu wa Vituo vya Polisi kutoka katika wilaya hizo mbili