********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Kutokana na wengi kupata maumivu makali pindi wanapolala kitandani, kituo cha kulea na kukuza ujuzi wa wahitimu wa VETA katika fani ya useremala na alminium kilichopo mtaa wa Mwembe Yanga Tandika Jijini Dar es Salaam(OSARIKO)kimetengeneza kitanda ambacho kinasaidia kupunguza matatizo kwa mwanadamu yanayosababishwa na namna tunavyolala.
Akizungumza Katika Maonesho ya 44 ya Biashara Katika vya Sabasaba vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Kituo cha SARIKO WOODWORK CO LTD, Bw.Oswin Komba amesema kuwa wameamua kutengeneza kitanda tiba kwaajili ya kuwaokoa wanaosumbuka na matatizo ya kupata maumivu pindi wanapoala.
“Namna tunavyolala katika vitanda vya kawaida kuna matatizo yanajitokeza kama vile maumivu ya mgongo,viungo,kiuno na shingo sasa matatizo hayo yanaweza kupungua kwa kutumia hiki kitanda tiba”. Amesema Bw.Komba.
Aidha Bw.Komba amesema kitanda tiba kinatumia godoro lenye unene wa nchi moja na nusu na juu ya godolo hilo unatandika kapeti huku chini ya godolo pia wameweka ubao ambao unaupokea mgogo unapolala unabakia katika hali yake ya kawaida.
“Wengi tunatumia magodolo yeye unene mkubwa na kutokana na unene ule tunapolala viungo vyetu vina athirika kutokana na kuwa na uneso mkubwa, uti wa mgongo unanepa na hivyo kusababisha pingiri za mgongo kupata maumivu”. Amesema Bw.Komba.
Pamoja na hayo Bw.Komba amesema mpaka sasa wameweza kukuza vipaji kwa vijana 20 na wengi wao wamejiajiri wenyewe na baadhi wameajiriwa kwenye sekta rasmi na zisizo rasmi.