Home Mchanganyiko Zingatieni haya kwenye Hospitali Mpya 28 – Dkt. Ntuli

Zingatieni haya kwenye Hospitali Mpya 28 – Dkt. Ntuli

0

Dkt. Ntuli Kapologwe, akifurahia Mfumo wa GoTHOMIS, uliyoboreshwa ijulikanayo kama GoTHOMIS Lite, katika kituo cha Afya Buzuluga cha Jijini Mwanza, ambapo mfumo huo umekuwa na tija katika uendeshaji wa shughuli za Afya nchini.. Moja ya Majengo ya Utoaji wa huduma za Afya likiwa linaoneka kuzingatia miundombinu ya wattu wenye ulemavu. Suala la Uboreshaji wa Hospitali na Vituo vya Afya linakwenda sambamba na uongezaji wa vifaa tiba, Hapa Dkt. Ntuli Kapologwe akikagua moja ya jengo la kutolea huduma pamoja na vifaa vyake.Moja ya Hospitali mpya 28 zilizopokea Milioni 500 kila moja kwaajili yakuanza ujenzi wa Hospitali za Wilaya, hapa zoezi la ujenzi likiwa limeanza.

*******************************

Na. Atley Kuni-OR-TAMISEMI

Mkurugenzi wa Afya na Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI, Daktari Ntuli Kapologwe, akiwa na jopo la wataalamu kutoka Ofisi hiyo, wamelazimika kutoa maelekezo muhimu yakuzingatia katika Hospitali mpya 28 za Halmashauri zinazoendelea kujengwa hivi sasa baada ya Halmashauri husika kupatiwa fedha na serikali kiasi cha milioni 500 za kuanzia.

Akifanya majumuisho hayo Dkt. Ntuli, amesema kwanza wamefurahishwa na utayari wa wanachi katika maeneo yao kwakujitolea kushiriki ujenzi huo unaoendeshwa kwa mtindo wa force account, kwani umeonesha mafaniko makubwa kote nchini, lakini akatahadharisha Kamati za Afya za Mikoa na Halmashauri, kuhakikisha zinaendelea kuwa bega kwa bega na timu za ujenzi shabaha ikiwa ni kuondokana na hatari yakukosewa kosewa kwa majengo hayo na hivyo kufanya kazi mara mbili lakini pia kuongeza gharama za ujenzi.  

Katika ziara hiyo iliyochukua muda wa siku 14, Dkt. Ntuli, amezitaka Kamati hizo kuhakikisha majengo yanazingatia ramani zilizopo lakini pale inapo lazimu kushauri, basi wasisite kufanya hivyo kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kutambua kasoro mapema.

Dkt. Kapologwe ameyataja maeneo ya kuta za Chumba cha Mionzi (X-Ray) kuwa zinatakiwa ziwe na unene usiopungua 300mm na Dirisha lake la kuingizia mwanga, liwe angalau Mita 2 kutoka kwenye floor Sehemu ya kuchukulia mionzi huku akitoa tahadhari kwa jengo hilo kuwekewa Aluminum au Grill na badala yake wazingatie kuwa eneo hilo litawekewa lead glass.

Amesema chumba hicho, kinatakiwa kuwa na mlango maalum ambao huwa unawekwa ili kuwazuia watoa huduma pamoja na wateja kutodhurika na mionzi itokanayo na mionzi isiyo dhibitiwa na kusema kwamba, wasitumie milango inayotumika katika nyumba zakuishi na badala yake watumie milango maalum na  

Dkt. Ntuli amesema sehemu za kufanyia kazi Works shop za Maabara zinatakiwa kuwa na Marbles na sio marumaru (tiles), aidha Marbles zilizopendekezwa ni vema zikawa na rangi nyeupe.

“Kwa upande wa Floor za Operating Theatre zinatakiwa kuwa na Epoxy mpaka eneo la sluice na sio marumaru za kawaida, huku akisema, madirisha ya Chumba cha upasuaji yanatakiwa kuwa na Grill Kwa nje na ndani, amesema Dkt. Ntuli, na kuzidi kusisitiza eneo la ndani kuwe na madirisha ya aluminium yasiyofunguka (fixed panels) na vioo viwe ni frosted glass, yaani visivyomuwezesha mtu wa nje kuona ndani.” Amesema, Mkurugenzi Ntuli.

Dkt. Ntuli, amesema pia mawasiliano kati ya Chumba cha kutakasia vifaa na Chumba cha Sluice liwekwe Dirisha na sio Mlango sambamba na tundu la nchi tatu ili kuweza kupitishia bomba la kutolea gas, pindi anapotakasa vyombo, amesisitiza mpangalio wa majengo vizuri ili kuwa na ufanisi wakati wa utoaji huduma, akitolea mfano, Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD)  linatakiwa kuwa uelekeo wa kuangalia Bara bara kuu na nyuma yake likifuatiwa na Jengo la Maabara.

Katika Majumuisho hayo Dkt. Ntuli amesema, Vituo vya kutolea huduma vinavyojengwa au karabatiwa vinatakiwa kuwa na tenki la kuhifadhia maji lenye uwezo wa ujazo usiopungua lita elfu 50, huku akipendekeza majengo yote yaunganishwe na Walk Way ili kurahisishia kazi kumtoa huduma  kutoka eneo moja kwenda eneo jingine.

Akiwa anahitimisha majumuisho hayo Dkt. Ntuli amesema, paa la Jengo la stoo ya dawa, linatakiwa kuwa na Materials maalumu ya kuzuia jotokali katika eneo husika, na kwa upande wa vyoo vya Walemavu, pamoja na maeneo yakupitia amesema kwamba, nilazima yawe na Supports pembeni kwa ajili ya kumsaidia mlemavu aendapo haja, vilevile akitaka, majengo yote sehemu ya kuingilia yawe na ramp kwa ajili ya Walemavu.

Mwisho Dkt. Ntuli, amesema katika chumba cha upasuaji milango yote inayoingia au kutoka wahakikishe   ni ya solid core flush doors, yenye spring hinges zinazofunguka pande zote, isiwe na vitasa bali push plates zilizofungwa pande zote za mlango.

Hivi sasa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, inaendelea na zoezi la ufatiliaji wa Hospitali 28 za Halmashauri ambazo zimewekwa katika mpango wa awamu ya pili ukitanguliwa na Hospitali 67 za awamu ya kwanza ambapo  tayari Hospitali 45 zimeanza kutoa huduma kwa wananchi hadi kufikia Mwezi Julai, 2020.