KAIMU Mkuu wa wilaya ya Pangani Godwin Gondwe kushoto akimkabidhi Kombe
Nahodha wa timu ya APL ya Kigombe ambao ni Mabingwa wa Ligi ya wilaya
ya Pangani Maarufu kama Aweso Cup kulia anayeshuhudia ni Mbunge wa Jimbo
la Pangani Jumaa Aweso (CCM) Ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akiwa ameshika
kitita cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kumkabidhi mshindi wa
mashindano hayo kushoto ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Pangani Godwin Gondwe
ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Handeni
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Pangani (CCM) akizungumza kwenye fainali ya Ligi ya Aweso
Cup
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif akizungumza wakati wa fainali hizo.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Pangani (CCM) akiwa amebebwa na baadhi ya wapenzi na
mashabiki wa soka wilayani Pangani mara baada ya kumalizika Ligi ya
Aweso Cup
Katibu wa Kamati ya Mipango na fedha wa Klabu ya Coastal Union Salim
Bawaziri kushoto akizungumza wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la
Pangani (CCM) na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Pangani (CCM) wa pili kutoka kushoto akiwa kwenye jukwaa
kuu na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Pangani Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu
wa wilaya ya Handeni kulia ni Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gipson
George wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye Ligi hiyo
Kikosi cha timu ya Wa2020 wakiwa kwenye Picha ya Pamoja
Kikosi cha timu ya APL ya Kigombe
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuhudhuria fainali hiyo
Sehemu ya mashabiki wa soka wilayani Pangani wakifuatilia mashindano hayo
Wapenzi na mashabiki wa timu ya APL ya Kigombe wakishangia ushindi huo
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye Ligi hiyo
NA MWANDISHI WETU, PANGANI.
TIMU ya APL FC ya Kigombe
wilayani Muheza mkoani Tanga imetawazwa mabingwa wapya wa Ligi ya wilaya
ya Pangani maarufu kama Aweso Cup baada ya kuifunga Wa 2020 FC mabao
2-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa soka Kumba.
Kutokana
na Ubingwa huo APL Kigombe walifanikiwa kukabidhiwa Kombe la Mashindano
hayo, Kitita cha Sh.Milioni moja na Ngom’be huku mshindi wa pili wa
2020 FC akipata kitita cha sh.laki sita na elfu sabini ya mbuzi na
medali za dhahabu.
Mshindi wa pili kwenye Mashindano hayo timu
ya Wa 2020 FC walikabidhiwa medali, kitita cha laki sita, mbuzi na
medali ya dhahabu kwa wachezaji wake huku mshindi wa tatu naye akipata
kitita cha sh.laki nne na mbuzi.
Mashindano hayo yamedhaminiwa
na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji huchezwa kila mwaka yakiwa na lengo la
kuibua na kukuza viwango vya soka mkoani humo ambayo yalishirikisha timu
16.
Mchezo huo wa fainali ya Ligi hiyo ulichezwa kwenye viwanja
vya Kumba mjini Pangani uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo
wasanii wa bongo movie.
Katika mchezo huo mabao ya APL ya
Kigombe ambao ndio mabingwa wapya yalifungwa na Malimo Magembe kwenye
dakika ya 35 baada ya kutumia uzembe wa mabeki wa timu pinzani kupachika
wavuni bao hilo.
Baada ya kuingia bao hiloWa 2020 FC waliweza
kurudi kujipan ga na kuanza kufanya mashambulizi ya mara kwa mara
langoni mwa APL ya Kigombe bila mafanikio kutokana na mashuti waliokuwa
wakijipa wachezaji wao kugonga mwamba na kutoka nje.
Shambulio hilo liliweza kuwaamsha APL Kigombe ambao baada waliweza kurudi kujipanga na kupelekea mashambulizi langoni
Akizungumza
kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi Naibu Waziri Aweso alisema
kwamba Ligi hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwani imewezesha
kupandisha timu nne kwenye Ligi ya mkoa na baadae anaamini zitafika Ligi
Daraja la kwanza na hatimaye Ligi kuu
Alisema kupitia michezo
wilaya ya Pangani inaweza kutoa wachezaji nguli kwenye soko kama vile
Mbwana Samata na Thomas Ulimwengi ambao wanaweza kuitangaza nchi kupitia
soka
Aidha aliwataka kuendelea kushikamana na kupendana huku
akikitaka Chama cha mpira wilayani Pangani kianzishe mashindanbo kwa
upande wa wanawake ikiwemo rede na mpira wa miguu atadhamini.
Kwa
upande wake Katibu wa Kamati ya Mipango na fedha wa Klabu ya Coastal
Union Salim Bawaziri alisema kwamba kupitia mashindano ya Aweso Cup
wameona vipaji vya wachezaji huku akieleza watachukua wachezaji 10 ambao
watawatumia kwenye Ligi kuu.