Mwanasheria wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Peace Mpango aweka saini mkataba huo.Wengine ni baadhi ya viongozi wa Mahakama, wakiwemo watumishi na wageni waalikwa.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Reli kutoka nchini China, Bw.Xie Zhixiang CRJE (East Africa) akisaini mkataba huo. Tukio hili limefanyika kwenye ofisi za Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania,Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru (katikati) jana alikabidhi mkataba wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Reli kutoka nchini China, Bw.Xie Zhixiang CRJE(East Africa).Jengo hilo litajengwa kwa muda wa miaka miwili, eneo la NCC Jijini Dodoma.( Kushoto) ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma na (kulia) ni Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Kevin Mhina.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru (katikati) jana Julai Mosi, mwaka huu, alisaini mkataba wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania na Mwenyekiti wa Kampuni ya Reli kutoka nchini China, Bw.Xie Zhixiang CRJE(East Africa) ambaye hayupo pichani .Jengo hilo litajengwa kwa muda wa miaka miwili, eneo la NCC Jijini Dodoma.( Kushoto) ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma na (kulia) ni Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Kevin Mhina.
Na Innocent Kansha- Mahakama
Mahakama ya Tanzania jana ilisaini mkataba wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama baina yake na Kampuni ya Reli kutoka China CRJE (EAST AFRICA) kwa makubaliano ya kukabidhi kazi hiyo ndani ya miezi 24.
Hafla hiyo imefanyika katika ofisi za makao makuu ya Mahakama Jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia kuhusu mkataba huo, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bw. Mathias Kabunduguru alisema anategemea muda waliokubaliana wa kupokea jengo hilo utakuwa kwa wakati muafaka na litaendanana na hadhi ya Muhimili husika.
‘‘Nategemea kuona tunapokea jengo zuri lenye ubora halisi unaoendana na thamani ya mkataba huu, kwani Mahakama ni moja ya nguzo ya Serikali hivyo hatutarajii kuona jengo lisilo lingana na hadhi ya Muhimili wenyewe,’ alisema Kabunduguru.
Aliongeza kuwa Mahakama ina wajibu wa kuhakikisha kila mtu anapata haki sio kwa Watanzania tu hata kwa wageni wanaofika hapa nchini kwa shughuli mbalimbali ikiwemo uwekezaji na Muhimili huo unatarajia kuwa na jengo hilo liwe chachu ya uharakishaji wa utoaji haki kama ilivyo katika jukumu lake la msingi la kikatiba.
Mtendaji huyo aliitaka ofisi ya Wakala wa Usimamizi wa Majengo Tanzania (TBA) itambue kwamba inayo wajibu wa kusimamia ujenzi huo sio kwa niaba ya Mahakama ya Tanzania bali kwa niaba ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwani Mahakama ni sehemu ya kiungo au Muhimili wa Serikali.
‘Mkandarasi unayo kazi kubwa mbele yako ya kuhakikisha unatekeleza wajibu wako ipasavyo ili uweze kupimwa kwa thamani ya jengo hili.
‘‘Niwakumbushe tu kwamba leo hii tumeingia kwenye jukumu kubwa na zito la kutia saini ujenzi huu tunategemea kuona sio tu kazi iliyo bora bali kazi inayotazamwa na Taifa zima kwa ujumla, hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha ujenzi huu unafanikiwa kwa kiwango kinachokidhi hadhi ya Mahakama,’’ alisisitiza.
Naye Mwenyekiti wa Kampuni ya Reli ya Nchini china CRJE (East Africa) Bw. Xie Zhixiang alihihakikishia Mahakama kuwa kampuni yao ina uzoefu mkubwa katika kutekeleza miradi mikubwa ya aina hii, hivyo wanategemea kujenga kwa kiwango cha ubora wa hali ya juu kulingana na makubalianao ya ujenzi huo.
Kwa upande wa Mkandarasi Mashauri, Wakala wa Majengo nchini (TBA), ambaye Msanifu wa Majengo Bw. Geofrey Munyaga alisema tunashukuru kwa kuaminiwa na serikali tupo tayari kutekeleza jukumu letu kikamilifu kama wasimamizi washauri katika mradi wa ujenzi huu tutahakikisha tunasimamia ubora wa ujenzi wa jengo hili unatekelezwa kama ilivyo kusudiwa na Serikali.
Mkataba wa ujenzi huo, umeanza leo na utakamilika ndani ya miaka miwili.