Baadhi ya
Watendaji wakifuatilia kwa kina kikao kazi na mkurugenzi wa
halmashauri hiyo Dkt.John Pima mapema jana katika ukumbi wa shuele ya
Arusha School picha zote na Ahmed Mahmoud ArushaNa Ahmed
Mahmoud Arusha
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt John
Pima,amewagiza watendaji wote wa kata na mtaa wa Jiji hilo
kuhakikisha wafanya biashara wadogo wana vitambulisho vya umachinga na waliyo na vitambulisho
wasibugudhiwe katika biashara zao ila watakaobainika
hawana vitambulisho hivyo kuwafungia kufanyabiashara.
Dkt
Pima ametoa maagizo hayo leo alipo kuwa akiongea na watendaji
wa kata na vijiji pamoja na wakuu wa idara
katika kikao mkakati cha utendaji kazi ili waweze
kubadilisha mwenendo wa utendaji kazi zao na kuwataka watendaji hao kuwa wazalendo katika taifa kwa kufanya
kazi zao kwa weledi wa hali ya juu kwa
kusimama katika majukumu yao.
“Hatuta cheka na mfanya
biashara yeyote asiyekuwa na kitambulisho cha umachinga na akisema hana pesa afunge biashara yake kwanza
mpaka atakapo pata pesa ya kulipia kitambulisho
pasipo hivyo hakuna kufanya biashara na pia nimepata taarifa
baadhi yenu watendaji mnakuwa na visingizio kwa sababu zenu
binafsi wenda mnafanya pia biasha hizo hizo”,Amesema Dkt Pima.
“Kwa wafanya biashara
wote wenye vitambulisho wasibugudhiwe kwa chochote kile na kuanzia kesho hakuna mtendaji kukaa ofisi
wote mwende kwa wananchi kuhakikisha yeyote
anayestahili kuwa na kitambulisho awe nacho
kuepusha changamoto zinazo weza mkuta kwasasa awamu ya tano inahitaji mtendaji anaye jitambua katika utendaji
kazi”,Aliongeza Dkt Pima.
Aidha pia Dkt Pima ameahasa
watendaji hao kutoweka visingizio vya mfumoko
wa kisiasa katika jiji la Arusha kwa kutotimiza wajibu wao
na kuwataka wasisjihushishe katika maswala
ya siasa badala yake wafanye kazi zao kwa weledi na kuacha na mambo
ambayo hayawahusi katika kazi zao za kuwatumikia wananchi na
kuwataka waelewe muelekeo wa serikali.
Awali
Watendaji hao wakitoa changamoto zilizo wafanya kutotimiza majukumu yao kwa kiwango kikubwa ni baada ya uongozi uliyo
kuwepo kuwaachia zoezi hilo la uuzaji wa
vitambulisho wenyewe hali iliyo pelekea zoezi hilo kuwa gumu
pia wananchi kulalamika kutokuwa na fedha za
kulipia vitambulisho hivyo kitu ambacho siyo cha kweli.
Katika zoezi la utoaji wa vitambulisho kwa wafanya
biashara wadogo hapa Nchini jiji la Arusha lilipewa
vitambulishe Elfu hamsi na nane nazoezi hilo la uuzaji wa
vitambulisho hilo kwa wafanya biashara linatakiwa kukamilika Julai 15 mwaka huu.
Ameahidi kuwa atawapa ushirikiano katika utendaji wake
kwa lengo la kusaidia kukaza mapato ya halmashauri
hiyo na kuendelea kuwaonya kutambua kwa kina malengo ya serikali ya
awamu ya tano kwani mmoja wenu akitokea hajui malengo hayo atupishe
kwani hawezi kwendana na kasi ya kukuza uchumi wan chi yetu huu
sio muda wa mtumishi kutojitambua ni kufanyakazi kwa mujibu wa
viapo vya maadili ya utumishi wa umma. |