Mkuu wa Masokowa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wasanii na wadau wa Sanaa wakati wa uzinduzi wa kipindi kipya cha Mahusiano cha ‘Date my Family’ jana. Kipindi hiki kinachoanza Julai 2, 2020, humuonyesha kijana katika hatua zake za kuchumbia kwa kuwasiliana na familia za wachumba watarajiwa na hatimaye kufanya maamuzi kabla hata hawajaonana. Muandaaji filamu maarufu nchini Aziz Mohamed akiwa na baadhi ya wasanii wenzake na wadau wa Sanaa wakati wa uzinduzi wa kipindi kipya cha Mahusiano cha ‘Date my Family’ jana. Kipindi hiki kinachoanza Julai 2, 2020, humuonyesha kijana katika hatua zake za kuchumbia kwa kuwasiliana na familia za wachumba watarajiwa na hatimaye kufanya maamuzi kabla hata hawajaonana. Aziz ni mzalishaji wa moja ya tamthilia maarufu nchini iitwayo HUBAMuigizaji maarufu wa Bongo Movie Hissan Muya ‘Stone’ akizungumza wakati wa uzinduzi wa kipindi kipya cha Mahusiano cha ‘Date my Family’ jana. Kipindi hiki kinachoanza Julai 2, 2020, humuonyesha kijana katika hatua zake za kuchumbia kwa kuwasiliana na familia za wachumba watarajiwa na hatimaye kufanya maamuzi kabla hata hawajaonana
*****************************
- Ni ‘Date My Family’ ambapo msaka mchumba huwasiliana na familia ya mchumba mtarajiwa
- Kipindi hicho kurushwa katika vifurushi vyote vya DStv kuanzia mwezi Julai
Kipindi cha kipekee cha mahusiano kijulikanacho kama ‘Date my family’ kitaanza kuonyeshwa DStv Chaneli ya Maisha Magic Bongo kuanzia Julai 2, 2020na kitaonekana katika vifurushi vyote na kitarushwa kila Alhamisi saa moja jioni.
Kipindi hiki cha aina yake cha mahusiano humuonyesha kijana katika hatua zake za kuchumbia lakini tofauti na ilivyozoeleka, hapa kijana atakuwa anawasiliana na familia za wachumba watarajiwa na hatimaye kufanya maamuzi ya mchumba kabla hata hawajaonana.
“Date My Familiy ni kipindi kinachohusu mahusiano hivyo kinawaunganisha watu wenye tabia zinazofanana ambapo kijana anayetaka mchumba atakutana na familia tatu tofauti zenye wachumba watarajiwa na baada ya mazungumzo na familia hizo mchumbiaji ataamua kumposa mchumba mmoja” amesema Ronald Shelukindo, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania.
Kulingana na mazungumzo ya kina baina ya mchumbiaji mwenyewe na familia ya mchumba, kijana atapata fursa ya kumfahamu vizuri mchumba wake bila kumuona. “Baada ya kukutana na familia hizo, mabachela au warembo hao watachagua familia waipendayo na hatimaye kwenda kukutana mchumba husika” alisema Shelukindo
Kipindi hiki kitakuwa ni burudani ya aina yake kwani kitakuwa na visa na Mikasa mingi kuanzia hatua ya kuongea na familia hadi hatua ya mwisho ya kukutanishwa na mchumba.
Kipindi hiki kinazalishwa hapa nchini na kampuni ya uzalishaji ya hapa Tanzania. Kampuni hiyo sio ngeni katika kutengeneza maudhui kwani ndiyo iliyoshiriki katika utengenezaji wa kipindi pendwa cha Harusi Yetu pamoja na Mwantumu ambavyo vyote vimejizolea umaarufu mkubwa hapa nchini.
“Kama ulivyo msisitizo wetu sisi Maisha Magic Bongo, asilimia kubwa ya maudhui yetu ni ya kitanzania na huzalishwa hapa na wazalishaji watanzania. Tunaamini kwa uzoefu wao watazalisha tena kipindi bora na kitakuwa burudani kubwa kwa watazamaji ndani nan je ya nchi”
“Jukumu letu kwa wateja ni kuhakikisha tunawapatia maudhui bora wakati wote na hivyo tunajitahidi kuleta vipindi vipya na vya kusisimua huku tukitumia wazalishaji maudhui wa ndani hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza tasnia yetu ya uzalishaji maudhui hapa nchini” alisisitiza Shelukindo.
Wakati kipindi hicho cha aina yake kikianza kurindima, Chaneli ya Maisha Magic Bongo inaendelea vipindi vingine vipya ambavyo vimeingia hivi karibuni ni pamoja na filamu za ‘Slayqueen’ na ‘Nyavu’ ambazo zimepata umaarufu mkubwa huku tamthilia maarufu ya HUBA na vichekesho vya Kitimtim nazo zikiendelea kuwaburudisha watazamaji wa DStv.
Kuhusu ‘Date My Family’
Date my family ni kipindi mahsusi cha mahusiano ambacho humuonyesha kijana katika hatua zake za kuchumbia lakini tofauti na ilivyozoeleka, hapa kijana atakuwa anawasiliana na familia za wachumba watarajiwa na hatimaye kufanya maamuzi ya mchumba kabla hata hawajaonana. Katika kipindi hiki kijana ataonana na familia tatu tofauti kabla hajafanya uamuzi huku wachumba hao watarajiwa wakishuhudia yanayojiri kwa njia ya mtandao.
Familia inamuelezea ndugu yao kwa undani zaidi hivyo kumpa nafasi mtu kuchagua kama anaweza kuingia kwenye mahusiano na mtu mwenye familia husika. Kwa kupitia mchakato huu, familia ndio itakayo changia kwa ndugu yao kupata mahusiano au vinginevyo.
Kuhusu Maisha Magic Bongo
Maisha Magic Bongo ni chaneli ya burudani inayotoa mchanganyiko wa maudhui yanayotengenezwa kwa soko la Tanzania . Maudhui haya ni mchanganyiko wa filamu, muziki, vichekesho, tamthilia, Makala na vipindi halisia. Chaneli hii inapatikana DStv chaneli 160.