Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Sanare (kushoto) akisikiliza kwa makini taarifa zilizokuwa zinawasilishwa na Watendaji juu ya kushindwa kutumia fedha za Ujenzi wa Madarasa na Jengo la Utawala Shule ya Sekondari SUA.
Baadhi ya wajumbe na walimu wa Shule ya Sekondari SUA iliyopo Manispaa ya Morogoro wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Loata Sanare alipofika shuleni hapo Juni 30,2020 kwa ajiri ya kutatua mgogoro Kati ya Kata ya Mbuyuni na kata ya Magadu zilizokuwa zinagombania Shule ya Sekondari SUA.
………………………………………………………………………
Na Farida Saidy,Morogoro
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare, amewataka Watendaji wa Taka kuacha tabia ya kuvutana wakati wa kutekeleza miradi ya maendeo Jambo ambalo linakwamisha Miradi ya Maendeleo kwa Wananchi.
Kauli hiyo ameitoa Juni 30, 2020 katika kikao cha kutatua mgogoro ulioibuka katika Ujenzi wa Madarasa na Jengo la Utawala katika Shule ya Sekondari SUA iliyopo Manispaa ya Morogoro,ambapo amewataka watendaji kufanya kazi kwa weledi na kuachana na migogoro isiyokuwa na maana.
Akizumnza katika kikao hicho kilichowakutanisha, Wajumbe wa Mabaraza mawili ya Kamati za Maendeleo kutoka Kata ya Magadu na Mbuyuni, wahandisi , pamoja na baadhi ya Wakuu wa Idara , waalimu pamoja na Uongozi wa Shule ya Sekondari SUA, RC Sanare, amewataka viongozi hao kutoa taarifa katika ofisi husika kuhusiana na changamoto za utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Aidha kutokana na kusuasua kwa ujenzi wa madarasa pamoja na Jengo la Utawala katika Shule ya Sekondari SUA, RC Sanare ametoa muda wa wiki mbili kukamilisha ukarabati wa ujenzi wa Madarasa na miezi miwili kukamilisha Ujenzi wa Jengo la Utawala.
“Nimekuja hapa baada ya kusikia kuna mvutano wa fedha baina ya kata hizi mbili yani Magadu pamoja na Mbuyuni, lakini maamuzi yangu yalikuwa mepesi sana, ningekuta mvutano huo bado unaendelea na hakuna maamuzi ninegemuomba Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kuichukua hiyo pesa na kuwaingizia watu wengine wenye uhitaji nazo”, alisema RC Sanare.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amesema katika kukomesha migogoro ya namna hiyo pesa zitakazokuja katika bajeti ijayo zitakuwa zinaingizwa moja kwa moja katika akaunti za Shule badala za Kata ili kuepusha migogoro ya namna hiyo.