Home Mchanganyiko VIONGOZI WA DINI KUWA MSTARI WA MBELE KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

VIONGOZI WA DINI KUWA MSTARI WA MBELE KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

0

………………………………………………………………………..

Na Farida Saidy,Morogoro.

KATIKA kukabiliana na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi Viongozi wa madhehebu ya dini wameishauri serikali kuangalia namna ya jamii kuzingatia maadili na misngi ya dini ikiwa ni pamoja na kudhibiti biashara ya ngono katika maeneo mbalimbali ambayo imekuwa kichocheo katika kusambaa kwa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.
 
Wakizungumza kwenye kikao kilichowakutanisha mashekhe kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Morogoro Shekhe Saidi Okasha ambaye ni mjumbe wa Baraza la Bakwata mkoa wa Morogoro na shekhe Salum Kirumba  wamesema kuwa viongozi wa dini wamekuwa wakipambana katika suala la uzingatiaji maadili lakini bado kuna changamoto katika masuala ya sera kudhibiti vitendo  vinayochechea kuenea kwa virusi vya ukimwi ikiwemo uvaaji mavazi yasiyofaa na biashara ya ngono.
 

Aidha wamesema Matarajio yao ni viongozi hao kusimamia mapambano dhidi ya  unyanyapaa unaodumaza juhudi za kutokomeza maambukizi ya VVU na ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto,  kwa viongozi hao kutumia nafasi zao kuelimisha waumini namna ya kujikinga na  kuambukizwa VVU.

 
 
 
Tanzania inakadiriwa kuwa na wastani wa watu million 1.6 wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, kati yao theluti mbili pekee ndio wanaotambua wana maambukizi, huku wengine wakiishi bila kujua hali zao, hivyo kuendelea kuwaambukiza wengine, huku viongozi wa Dini wakitazamwa kuwa dira, kuifikia Tanzania bila maambukizi mapya ifikapo 2030.