Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu akizungumza wakati akitoa mchango wa mabati 1000 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za matawi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zaidi ya 40 katika Wilaya ya Ikungi.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu akitoa msaada wa mabati 1000.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu akitoa msaada wa pikipiki.
Na Mwandishi Wetu, Singida
MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu ametoa mchango wa mabati 1000 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Matawi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zaidi ya 40 katika Wilaya ya Ikungi.
Mbali ya kutoa mabati hayo Mtaturu ametoa tenki la maji, pikipiki mbili kwa ajili ya matumizi ya kiofisi kwa makatibu na moja kwa Msikiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Wilaya ya Ikungi vyote vikiwa na thamani ya shilingi 30.270,000.
Mchango huo ni muendelezo wa jitihada zake za kukiimarisha chama kilichomuamini na wananchi kumpatia ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo.
Aidha Mtaturu amekabidhi pikipiki moja kwa ajili ya matumizi ya Chama Cha Mapinduzi katika wilaya hiyo.
Akikabidhi vifaa tu hivyo Mtaturu alisema anatekeleza ahadi yake aliyoahidi wananchi ambapo amewataka wanufaika wa vitu hivyo kuhakikisha wanavitunza na kuendelea kuiamini Serikali iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.