Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa ili kuzindua mradi mkubwa wa maji wa Kibamba-Kisarawe katika sherehe zilizofanyika Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani leo tarehe 28 Juni 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungua maji kwenye eneo la mradi wa Kibamba -Kisarawe mkoani Pwani mara baada ya kuzindua mradi huo mkubwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishika maji ya bomba mara baada ya kuzindua mradi mkubwa wa Maji wa Kibamba-Kisarawe mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na viongozi mbalimbali mara baada ya kuzindua mradi mkubwa wa Maji wa Kibamba-Kisarawe mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungua bomba kwa pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Mtendaji Mkuu wa Dawasa Eng. Cyprian Luhemeja, Mwenyekiti wa Bodi ya Dawasa Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia Wafanyakazi wa Dawasa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Mkutano mara baada ya kuzindua mradi wa maji wa Kibamba Kisarawe uliogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 10.6.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakati wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Dawasa Eng. Cyprian Luhemeja wakati alipokuwa akitoa maelezo ya miradi mbalimbali ya Maji katika mkoa wa Dar es Salaam na Kisarawe mkoani Pwani. PICHA NA IKULU
………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Dkt John Pombe Magufuli amezindua mradi wa maji wa Kibamba Kisarawe uliotekelezwa na Mamlaka ha Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA.
Mradi huo umejengwa kufuatia agizo alilotoa Juni 21,2017 wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa Ruvu Juu akiwataka Dawasa kutanua mtandao wa Usambazaji maji na kupeleka maji Kisarawe.
Akitoa maelezo ya mradi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mradi wa Kisarawe umejengwa kwa fedha za ndani Bilion 10.6 zinazotokana na makusanyo ya maduhuli ya mauzo ya maji.
Luhemeja amesema wakati wa utekelezaji wa mradi huo, Dawasa iliona fursa ya kujenga mradi mwingine wa Bilionj 7.3 wa kuyatoa maji katika tenki la Kisarawe linalohifadhi maji Lita Milioni 6 kupeleka katika maeneo ya Dar es Salaam.
Amesema, kukamilika kwa mradi wa maji Kisarawe umewezesha maunganisho mapya yapatayo 1650 na bado wanaendelea kufanya maunganisho mapya na wananchi wanaendelea kupata maji safi.
Aidha, maeneo yatakayonufaika na mradi huo ni Kata za Kisarawe, Kazimzumbwi, Kiluvya, Kwembe, Kisopwa, Mloganzila na maeneo maalumu ya Viwanda.
Akizungumzia upatikanaji wa hali ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam, Luhemeja amesema kwa sasa asilimia 88 wanapata maji kutoka asilimia 68 mwaka 2015 kwahiyo ni ongezeko kubwa la maji.
Pia lengo la Dawasa ni kuona kufikia mwaka 2025, asilimia 95 wanapata maji safi katika muda wote.