Home Mchanganyiko MANENO YA WAZIRI JAFO MBELE YA RAIS MAGUFULI WAKATI WA UZINDUZI MRADI...

MANENO YA WAZIRI JAFO MBELE YA RAIS MAGUFULI WAKATI WA UZINDUZI MRADI WA MAJI WA KIBAMBA-KISARAWE

0
……………………………………………………………………………
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemeani Jafo amemshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kumuamini na kumteua kwenye nafasi hiyo ya uwaziri licha yeye ni fundi selemala huku akimhakikishia kuendelea kufanya kazi kwa juhudi zake.
Jafo amesema hayo leo  wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wilayani Kisarawe ambapo Rais Magufuli ameuzindua rasmi na hivyo kutatua changamoto ya tatizo la maji ambalo limewakabili kwa muda mrefu wananchi wa Kisarawe mkoani Pwani.
“Mheshimiwa Rais Magufuli , hakika binafsi nakushukuru sana kwa kuniteua kwenye nafasi hii, mimi sio chochote, sio lolote lakini kwa jicho lako mwenyewe uliamua kuniteua kuwa Waziri katika ofisi yako.Mimi ni fundi selemala na wale ndugu zangu wa ambao tumeanzisha mji wa Njiro pale Arusha wananifahamu kama fundi Selemala lakini Rais Magufuli ameamua kuniteua.
“Nikuhakikishie Rais , nitaendelea kufanya kazi kwa nguvu, maarifa na juhudi zangu zote kubwa kadri ya maelekezo yako kwa nia njema ya kuleta maendeleo ya Watanzania wote wakiwamo wana Kisarawe.Nakumbuka katika mkutano wako na viongozi wa dini uliwaambia wanichunge mpaka 2015, na kweli wamefanya hivyo, ahsante Rais,
“amesema Jafo.
Kuhusu wilayani Kisarawe Jafo amesema kuwa moja ya changamoto kubwa ilikuwa ni changamoto ya upatikanaji wa maji lakini hatimaye chini ya Rais Magufuli leo hii wananchi wanashuhudia mradi mkubwa maji ukilizunduliwa wenye thamani ya Sh.bilioni 10.6 na hivyo kwenda kutatua changamoto hiyo.
Mbali ya changamoto ya maji, Waziri Jafo amesema katika elimu kulikuwa na shule moja tu ya kidato cha tano na sita ya Minaki lakini hivi sasa kuna shule nyingine za kidato cha tano na sita wilayani humo na mbil tayari zimeanza kupokea wanafunzi.
Wakati katika sekta ya afya, nako vituo vya afya vimejengwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kisarawe na hivyo kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.Pia amezungumzai ujenzi wa miundombinu ya barabara ambapo chini ya Rais Magufuli barabara za wilaya hiyo nyingi zimeboreshwa na zinapita wakati wote.
Waziri Jafo amesema kutokana na mambo makubwa ya maendeleo ambayo yamefanyika wilayani Kisarawe, Rais Magufuli katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu asiwe na wasiwasi kwani wananchi wa Wilaya hiyo wameshaamua Rais ni Magufuli.
“Rais Magufuli nikuhakikishie huku kwa watani zako wameshamua katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni wewe.Ukija huku wakati wa kampeni wewe njoo tu upite kwa ajili ya kutusalimia lakini biashara ya uchaguzi mkuu biashara ilishakwisha tunasubiri kupiga kura tu,”amesema Waziri Jafo.