Meneja Mkazi wa SAMIRO Pharmaceutical ltd Masila Mani akimkabidhi zawadi Kaimu Kamanda wa Polisi Kikosi cha Afya SSP Dk. Gerald Magesa ambaye pia ni afisa Mnadhimu mkuu wa kikosi.
Meneja Mkazi wa SAMIRO Pharmaceutical ltd Masila Mani akimkabidhi zawadi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Polisi Kilwa Road SP. Dk. Cleophace Mtana.
Meneja Mkazi wa SAMIRO Pharmaceutical ltd Masila Mani akimsikiliza SSP Abdalla Mpalilo wakati akitoa shukurani zake kwa niaba ya Hospitali hiyo.
Meneja Mkazi wa SAMIRO Pharmaceutical ltd Masila Mani akisungumza jambo huku daktari Stephen Kisaka kutoka ofisi ya Mipango na Utafiti Idara ya Elimu ya Afya Kilwa Road Hospital akimsikiliza.
Mfamasia Bw.Daud Godfrey kutoka Samiro Pharmaceuticals ltd akifafanua jambo katika semina hiyo.
Baadhi ya wataalamu wa afya katika hospitali ya Polisi ya Kilwa Road wakimsikiliza Meneja Mkazi wa SAMIRO Pharmaceutical ltd Bw,Masila Mani wakati akiwasilisha mada kuhusu virutubisho wa Life Gain.
Meneja Mkazi wa SAMIRO Pharmaceutical ltd Masila Mani akimsikiliza Mfamasia Bw.Daud Godfrey kutoka Samiro Pharmaceuticals ltd wakati alipokuwa akitoa mada katika semina hiyo.
Meneja Mkazi wa SAMIRO Pharmaceutical ltd Masila Mani akifafanua jambo katika semina hiyo iliyofanyika jana katika hospitali ya Polisi ya Kilwa Road jijini Dar es salaam.
………………………………………………….
Umri wa uzeeni ni umri ambao upo katika hatari zaidi ya kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama magonjwa ya moyo, figo ,kisukari na kansa. hivyo Samiro Pharmaceutical ltd kwa kuliona hili ili imeamua kuja na tiba lishe ambayo inaitwa Life Gain kwa ajili ya kuwasaidia watu kupata virutubisho vya ziada wakati wanapopitia katika magonjwa ama mitindo ya maisha ya kila siku.
Hayo ameyasema Meneja Mkazi wa SAMIRO Pharmaceutical ltd Masila Mani wakati akizungumza katika semina ya wataalamu wa afya iliyofanyika katika Hospitali ya Polisi ya Kirwa Road jijini Dar es salaam jana.
Masila Mani amesema Life Gain ni lishe ambayo ipo katika hali ya unga ama poda inapatikana katika ladha mbili ambazo ni Vanilla na (Strawbberry).Life Gain imetengenezwa na kuhifadhiwa vizuri katika makopo na vifungashio vingine ambavyo vinapatikana katika ofisi za maduka yao ya dawa yaliyopo Kariakoo pamoja na maduka mengine yaliyopo maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.
Bw. Masila Mani amesema umuhimu wa Life Gain na matumizi yake anaweza kutumia mtu yeyote anayefanya mazoezi na michezo kwa ajili ya kumuongezea nguvu na kuimarisha misuli ya mwili.
Amesema pia anaweza akatumia mtu mwenye ugonjwa wa kisukari kwa kuwa Life Gain imetengenezwa bila kuwekwa sukari ndani yake na ina Fiber(Nyuzi Nyuzi) ambazo humsaidia mgonjwa wa kisukari kutojisikia kula mara kwa mara hii humsaidia kurekebisha kiwango chake cha sukari mwilini.
Ameongeza kuwa kirutubisho hicho husaidia watu wenye matatizo ya moyo kupata virutubisho stahiki kwa kuwa Life Gain ndani yake kuna kiwango kidogo cha sodium (Chumvi ya mezani) 167mg per100g.
“Kiwango hiki kidogo cha (Sodium) husaidia kupunguza Presha ya damu, Kupunguza pia hatari ya kupata Kansa ya Tumbo ambapo tafiti pia zinaonyesha ongezeko la (Sodium) mwilini huleta hatari ya kupata ugonjwa sugu wa Figo”.Amesema Masila Mani.
” Mtu mwenye HIV/UKIMWI anaweza kuitumia hii pia kwa kuwa ndani yake kuna Protein,Zinc, Vitamins zote muhimu na madini yote muhimu yanayohitajika katika mwili wa binadamu, Kama tunavyojua watu ambao kinga zao za mwili zimeshuka hata mmeng’enyo wao wa chakula unakuwa hauko vizuri kwa hyo wakila vitu vyenye sukari na mafuta wana tabia ya kuharisha na kutapika”.Ameongeza Manila mani.
Life Gain haikuwekwa sukari na mafuta kwa ajili ya watu wa aina hii. hii husaidia mgonjwa kuimarika kinga ya mwili ,kutengeneza (Tissue) zilizoharibika na kupunguza “inflammation”.lakini pia Life Gain inapunguza athari za kupata magonjwa sugu ya figo kwa kuwa ndani yake kuna kiwango cha Magnesium 255.mg asilimia 100.
Life Gain pia inaweza kumsaidia mama mjamzito kuongeza damu kwa kuwa ina madini ya chuma na Folic Acid ,uwepo wa Fiber humsaidia mama mjamzito kupata choo laini ,kutokuwepo kwa mafuta humsaidia mama mjamzito kutokujisikia kutapika kipindi anapoitumia. Life Gain, pia anaweza akatumia mgonjwa wa ICU ambaye anahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari kumuongezea kinga,nguvu na kumsaidia katika mmeng’enyo wa chakula wagonjwa wengi wa ICU hushindwa kula wenyewe hivyo hutumia mipira kulishwa chakula.
Kwa sababu Life Gain imetengenezwa kwa unga laini unaweza hutumika kumlisha mgonjwa kwa njia ya mpira akala bila tatizo lolote. lakini mwisho hii Life Gain anaweza akatumia mtu yeyote ambaye ametoka kuumwa na kukosa hamu ya kula inamsaidia mgonjwa kupata hamu ya kula.
Masila Mani ameelezea namna mgonjwa anavyoweza kuitumia Life Gain ambapo atatakiwa kuchanganya kiasi cha maji kwa kuchukua vijiko viwili vya unga wa Life Gain anachanganya kisha unakunywa. mgonjwa anaweza akaitumia kwa siku mara mbili ama mara moja.vijiko viwili ni sawa na 30gm.
“Wengine hupenda kuchanganya kwenye aina mbali mbali za Juice ,Maji ya moto na maziwa fresh.Kwa kuwa asilimia kubwa ya watanzania hawazingatii upangiliaji na ulaji wa vyakula bora,hivyo basi uwepo wa Life Gain utasaidia kaleta uimarishaji wa lishe bora na afya bora miongoni mwa watanzania