**************************
NA EMMANUEL MBATILO
Chelsea imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji raia wa Ujerumani, Timo Werner ambaye amesajiliwa akitokea klabu ya RB Leipzig kwa dau la paundi milioni 47.5.
Nyota huyo mwenye miaka 24 amesaini mkataba wa miaka mitano klabuni Chelsea na atapokea mshahara wa paundi 170,000 (Tsh. milioni 492) kwa wiki.
Timo Werner anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa chini ya utawala wa kocha Frank Lampard uku pia akisajiliwa wakati dirisha la usajili halijafunguliwa kama alivyosajiliwa Hakim Ziyech.
Atajiunga na Chelsea pale tu msimu wa ligi kuu Ujerumani utakapomalizika.