Home Mchanganyiko MAMILIONI YATENGWA KUENDELEZA WASHINDI 70 WA MAKISATU

MAMILIONI YATENGWA KUENDELEZA WASHINDI 70 WA MAKISATU

0

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma wakati akitangaza washindi wa mashindano ya Kitaifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU)  yaliyofanyika Machi 16 hadi Machi 20 mwaka huu.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi.Sylvia Lupembe,akimkaribisha Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla hajaanza kutoa taarifa za washindi wa mashindano ya Kitaifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU)  yaliyofanyika Machi 16 hadi Machi 20 mwaka huu.

…………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa SERIKALI imetenga kiasi cha shilingi 750 milioni kwa ajili ya kuwaendeleza washindi 70 wa mashindano ya ubunifu wa Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yaliyofanyika Machi 16 hadi Machi 20 mwaka huu.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema fedha hizo zitatumika kuwaendeleza wavunifu hao ili kazi zao ziwe kibiashara na kuwainuabkiuchuni.

Aidha Prof. Ndalichako amesema kuwa Serikali itaendelea kutenga fedha zaidi mwaka hadi mwaka kwa ajili ya kuendeleza bunifu mbalimbali nchini.

“Natoa rai kwenu na washindi wote kuendeleza bunifu zenu ili kuhakikisha zinakuwa fursa za kiuchuni kwenu”, ametoa wito Prof. Ndalichako.

Prof. Ndalichako amesema,Serikali imetoa shilingi milioni 5 kwa washindi wa kwanza katika makundi yote ,shilingi milioni 3 kwa washindi wa pili kwa makubdi yote na shilingi milioni 2 kwa washindi wa tatu katika makundi yote.

Makundi yaliyoshiriki katika mshindano hayo ni pamoja na shule za msingi,  sekondari,vyuo vya ufundi stadium,vyuo vya ufundi wa kati,vyuo vikuu ,taasisi za utafiti na maendeleo pamoja na Mfumo usio rasmi