Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Singida Mjini, wakimpongeza Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe (kulia) kwa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015-2020.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alexandrina Katabi, akizungumza katika mkutano huo.
Katibu wa UWT Singida Mjini, Maimuna Likunguni, akiendesha mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Singida, George Silindu, akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Mwanahamisi Itua, akizungumza.
Katibu wa UWT Mkoa wa Singida, Edina Kuguru, akizungumza.
Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Singida Mjini, wakimpa zawadi Mbunge wao Aysharose Mattembe.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe ametoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho ndani ya uongozi wake kwa kipindi cha miaka mitano kwa UWT Wilaya ya Singida Mjini.
Akikabidhi taarifa hiyo juzi kwa Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Singida Mjini, Mattembe aliwapongeza wanawake wa umoja huo kwa ushirikiano uliopelekea ushindi kwenye chaguzi ndogo zilizofanyika kwenye wilaya hiyo.
Alisema UWT ndio waliomfanya afike hapo alipo pamoja na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa ilani ndani ya Wilaya hiyo na Mkoa kwa ujumla,huku akimshukuru Rais kwa kupeleka miradi ya maendeleo kwenye Mkoa huo.
“Namshukuru Mh.Rais kwa kutuletea na kutekeleza miradi mingi katika manispaa yetu,lakini pia nampongeza ujasiri alionao uliopelekea kuwaondolea hofu wananchi baada ya kukumbwa na janga la ugonjwa wa Corona.” alisema Matembe.
Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alexandrina Katabi aliwaomba wanawake hao kuendelea kusimamia umoja na mshikamano walionao na kuhakikisha CCM inashinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Katibu huyo alisisitiza na kuwaomba wanawake hao kujitokeza kupiga kura pamoja na kuhamasisha watu wengine wanaowazunguka kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi unaokuja hapo baadaye mwaka huu.
“Kila mmoja kwa nafasi aliyonayo kuhakikisha anajipanga katika uchaguzi huu ili CCM Mkoa wa Singida ishinde kwa asilimia mia moja.” alisema.
Amewakumbusha kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali lakini kukubali na kuwaunga mkono wale watakao chaguliwa hata kama yeye hajapata nafasi ya kuchaguliwa.
“Kwenye siasa unapoamua kugombea nafasi yoyote lazima ukubali matokeo mawili kushindwa na kushinda, katika hili lazima tushirikiane,tukigawanyika hatutashinda.” alisema.