Home Siasa MAKADA WA CCM WACHUKUA FOMU ZA KUWANIA URAIS WA ZNZ

MAKADA WA CCM WACHUKUA FOMU ZA KUWANIA URAIS WA ZNZ

0

KATIBU wa NEC,Idara ya Oganazesheni CCM Zanzibar Cassian Galos Nyimbo (kushoto),akimkabidhi fomu ya kuwania kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Kada wa CCM Balozi Ali Abeid Amani Karume(kulia) huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwanduzi Zanzibar.

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Mbwana Bakari Juma aliyechukua fomu ya kugombea Urais kupitia CCM akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kuwania Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi.

Katibu wa NEC,Idara ya Oganazesheni CCM Zanzibar Cassian Galos Nyimbo (kushoto), akimkabidhi fomu Kada wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Ndugu Mbwana Bakari Juma(kulia) aliyechukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais kupitia CCM, huko Afisi Kuu ya CCM Kiwandui Zanzibar.

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Mbwana Bakari Juma aliyechukua fomu ya kugombea Uraiswa Zanzibar kupitia CCM, akipewa maelezo na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Oganazasheni Ndugu Abdi Mahmoud Abdi (kulia)  baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, ambapo kushoto ni Katibu wa NEC,Idara ya Oganazesheni CCM Zanzibar Cassian Galos Nyimbo.

KADA wa CCM Balozi Ali Abeid Amani Karume aliyechukua fomu ya kuwania kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar akionyesha mkoba wenye fomu hiyo mada baada ya kukabidhiwa huko Afisi Kuu CCM Zanzibar.

KADA wa CCM Balozi Ali Abeid Amani Karume akiwa katika picha mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, hafla hiyo imefanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.