Diwani wa Kata ya Kibamba aliyemaliza muda wake wa miaka mitano tangu kupitia tiketi ya Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Ernest Mgawe kushoto akimkabidhi mmoja wa viongozi wa kata wa chama hicho ripoti maalumu ya utekelezaji wa majukumu mbali mbali ambayo aliyafanay wakati wa uongozi wake kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2015/2020 katika halfa ambayo ilihudhuliwa na viongozi mbali mbali.(Picha na Victor Masangu)
Diwani aliyemaliza muda wake Kata ya Kibamba Ernest Mgawe kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) akiwaonyesha ripoti yake ya utekelezaji katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake (Picha na Victor Masangu)
Diwani wa kata ya Kibamba ambaye amemaliza muda wake kupitia tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo (C akizungumza na viongozi wa chama hicho pamoja na wanachama wakati wa halfa fupi ya (CHADEMA) Ernest Magawe akisoma ripoti yake ya utekelezaji wa majukumu tangu alipochaguliwa mnamo mwaka 2015 /2020 (Picha na Victor Masangu).
Mke wa Diwani wa kata ya Kibamba aliyemaliza kipindi cha muda wake akitoa neon la shukrani mara baada ya kumalizika kwa halfa hiyo ya kutoa ripoti ya utekelezaji wa majukumu yake wakati wa kipindi chake cha uongozi kuanzia mwaka 2015 hadi 2020.(Picha na Victor Masangu)
**********************************
NA VICTOR MASANGU, KIBAMBA
Diwani wa kata ya Kibamba aliyemaliza muda wake wa kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Ernest Mgawe amekabidhi ripoti maalumu kwa uongozi wa chama chake ambayo imetaja vipaumbele 14 vya msingi ambayo amevitekeleza wakati wa uongozi wake kuanzia kipindi cha mwaka 2015/2020 katika sekta mbali mbali ikiwemo afya, elimu, maji pamoja na miundombinu ya barabara.
Akizungumza katika halfa fupi ambayo iliandaliwa kwa ajili ya kukabidhi ripoti hiyo kwa uongozi wa chama ngazi ya Wilaya pamoja na viongozi wengine waandamizi kutokea kwenye mitaa mbali mbali alisema kwamba ripoti ndani ya ripoti hiyo imeweza kuelezea mambo mbali mbali ya kimaendeleo ambayo yalifanyika katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tangu kuchaguliwa kwake.
Mgawe alibainisha kwamba anamshukuru mwenyezi Mungu kwa kuweza kumsaidia katika kutekeleza majukumu yake katika kipindi chote kwa kushirikiana bega kwa bega na viongozi wake wa chama kwa lengo la kuweza kuwalatea mabadiliko chanya wananchi wa kata ya kibamba katika Nyanja mbali mbali lengo ikiwa ni kutimiza zile ahadi ambazo alizitoa kabla ya kuchaguliwa kwake.
“Katika miaka mitano ya uongozi wangu kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka huu wa 20202 tumeweza kwa kweli kushirikiana na wanananchi wa kibamba katika maeneo mbali mbali na pia nina imani kuwa upendo wao na ushirikiano wao ambao walinipatia katika kipindi chote ndio umeweza kunifukisha hapa hadi nimemaliza kipindi changu salama hivyo nina imani siku zote mafanikio hayawezi kuja pasipo kuwa na kuwa na ushirikiano baina na uongozi pamoja na wananchi wenyewe.,”alisema Mgawe.
Aidha alisema kuwa wakati wa kipindi chake cha uongozi aliweza kushiriki kikamilifu katika shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo kuchangia ujenzi wa nyumba za ibada, sambamba na kutoa misaada mbali mbali katika kuwasaidia baadhi ya wananchi katika masuala ya matibabu kwa ambao walikuwa na changamoto ya kutojiweza katika gharama sambamba na kuwahudumia wajane.
Katika hatua nyingine alisema kwamba katika kuhakikisha kwamba suala la ulinzi na usalama linaimarishwa kwa wananchi wake na kuondokana na wimbi la uharifu na unyanganyi alishirikiana kwa dhati na jeshi la Polisi katika kufanikisha ujenzi wa kituo cha polisi ambacho kilijengwa katika maeneo ya gogoni ambacho kimeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa mambo ya uharifu.
Pia Diwani huyoa aliyemaliza muda wake kalisema kwamba katika upande wa miundombinu ya barabara kila mwaka anahakikisha barabrara zinazotumiwa na wananchi wengine zinafanyiwa ukaarabati wa kina ikiwemo kuziwekea vifusi pamoja na zile nyingine za mitaani kuchongwa ili ziweze kupitika kwa urahisi hasa katika kipindi cha mvua zinaponyesha.
Diwani huyo alielezea kwamba kulikuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji pindi alipoingia madarakani hivyo aliamua kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha anamaliza kero ya maji kwa wananchi wa kata ya kibamba hasa katika maeneo ya mtaa wa kibwegere ambao ulikuwa na shida hiyo lakini kwa sasa serikali imeshatenga bajeti kwa ajili ya usambazaji wa msji katika maeneo mbali mbali.
Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 Diwani huyo aliyemaliza muda wake aliweza kutekeleza majukumu yake mabali mbali ikiwemo kuleta huduma bila ya ubaguzi, kushiriki katika shughuli za kijamii,kuwahudumia wajane,ulinzi na usalama,miuundombinu ya barabara, huduma ya maji, umeme,ardhi.afya, elimu pamoja mutatua migogoro ndani ya kata.