***********************************
Na.Mwandishi Wetu -Arusha
Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) kupitia Ofisi ya Afisa Mwandikishaji ambae ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha imesema kuwa itaweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura kwa siku nne mfululizo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha pamoja na wawakilishi wa Vyama vya Siasa mkoani Arusha,Afisa Uandikishaji Msaidizi wa Jiji hilo bwana Misena Bina,alisema daftari litakuwa wazi kuanzia June 17-20, katika vituo vilivyotumika awali wakati wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Aidha alisema kuwa Wakati wa zoezi hilo la uwekaji wazi litafanyika kwa kuzingatia tahadhari zote za Afya kuhusu kuzuia maambukizi ya Ugonjwa wa Covid-19,unaosababishwa na Virusi vya Corona.
“Wahusika ni Wapiga Kura wote walioandikishwa katika daftari la kudumu,la wapiga Kura mwaka 2015,walioandikishwa wakati wa Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura Awamu ya kwanza na ya Pili kwa mwaka 2019/2020″alisema bwana Bina.
“Wapiga kura Hawa ni wale ambao hawakuhakiki taarifa zao, wakati wa uwekaji wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura Awamu ya kwanza,Wapiga Kura watakaohakiki taarifa zao kwenye Daftari la Awali la Wapiga Kura lolipowekwa wazi na kukuta picha zao hazipo mwanatakiwa kwenda shule ya msingi Meru,karibu na kituo Cha Afya Kaloleni ili wapigwe picha nyingine haraka”alisema bwana Bina.
Hata hivyo alisema kuwa Mambo ya kuzingatia ni Daftari la Awali la Wapiga kura litabandikwa katika vituo vyote vilivyotumika kuandikisha Wapiga kura.
Nae Afisa Uchaguzi wa Jiji la Arusha bi.Namyaki Naitetei alisema kuwa Pingamizi zote zitawekwa kwa vielelezo na ushahidi na sio maneno matupu.
Pia aliwataka Wapiga kura kutoa taarifa za ndugu waliofariki dunia ili waondolewe kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura.
“Nataka niwaambie zoezi hili hakutakuwa na uandikishaji wa Wapiga kura wapya,Aidha hakutakuwa na Uboreshaji wa taarifa za Wapiga kura waliohama maeneo ya kiuchaguzi waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika”alisema bi.Namnyaki.
Bi.Namnyaki aliwataka wakazi wa Jiji la Arusha kuzingatia kanuni za Afya kwa kufuata maelekezo watakayopewa wawapo vituoni,ili kujiepusha na maambukizi ya Virusi vya Corona.