Mkuu wa Idara ya masoko wa Dstv Baraka Shelukindo (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni ya Tigo na Dstv utakaowawezesha wateja wa kampuni hizo kushuhudia michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vifurushi vya gharama nafuu. Kushoto ni Mkuu wa Huduma na bidhaa wa Tigo David Umoh na kulia ni Mtaalamu wa Huduma za Intaneni wa Tigo Allen Salaita.
Mkuu wa Huduma na bidhaa wa Tigo David Umoh (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni ya Tigo na Dstv utakaowawezesha wateja wa kampuni hizo kushuhudia michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vifurushi vya gharama nafuu. Kulia ni Mkuu wa Idara ya masoko wa Dstv Baraka Shelukindo na kushoto ni Mtaalamu wa Huduma za Intateni wa Tigo Allen Salaita.
Mkuu wa Huduma na bidhaa wa Tigo David Umoh (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni ya Tigo na Dstv utakaowawezesha wateja wa kampuni hizo kushuhudia michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vifurushi vya gharama nafuu. Kulia ni Mkuu wa Idara ya masoko wa Dstv Baraka Shelukindo na kushoto ni Mtaalamu wa Huduma za Intateni wa Tigo Allen Salaita.
Mkuu wa Huduma na bidhaa wa Tigo David Umoh (kushoto) akiwa na Mkuu wa Idara ya masoko wa Dstv Baraka Shelukindo (kati kati) na Mtaalamu wa Huduma za Intaneni wa Tigo Allen Salaita wakipongezana baada ya uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni ya Tigo na Dstv utakaowawezesha wateja wa kampuni hizo kushuhudia michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vifurushi vya gharama nafuu.
******************
Na Mwandisi Wetu Wateja wa Tigo na DStv sasa wataweza kufurahia mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika mubashara wakiwa sehemu yeyote na kwa muda wowote, baada ya makampuni haya mawili kuzindua ushirikiano maalum na mahususi ya huduma ya DStv itakayowapa wateja wake fursa ya kutazamaa mechi hizo kupitia DStv Now mobile App kwa gharama nafuu.
Akizungumzia na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huo, tMkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh alisema ushirikiano huo na DStv unaendana sambamba na lengo la kampuni hiyo kukuza maisha ya kidijitali kwa kila Mtanzania.
.
“Tunayofuraha ya kuzindua huduma hii maalum ya DStv Now itakayowapa wateja wetu wa Tigo katika msimu huu wa michuano ya Afrika kupata fursa nzuri ya kutazama mechi mtandaoni na kushuhudia timu yao pendwa ya Taifa Stars na timu nyingine zinazoshiriki mashindano haya makubwa barani Afrika,” alisema Umoh.
Aliongeza, “Kupitia mtandao wetu bora wa 4G, tunaweza kuwahakikishia wateja wetu wanaotumia DStv fursa ya uhakika ya kuunganishwa mubashara na bila usumbufu wowote kuangalia Kombe la Mataifa ya Afrika, kutoka sehemu yeyote na muda wowote kupitia DStv Now App katika vifaa walivyonavyo. Hii ni fursa nzuri pia kwa wale wateja ambao kwa sababu mbalimbali hawatakuwa na nafasi ya kutazama kupitia televisheni zao.”
Kwa mujibu wa Umoh, Tigo inawapa wateja wake waliounganishwa na DStv nafasi ya kuchagua vifurushi vitatu. Cha kwanza ni kifurushi cha GB 1.5 kwa gharama ya TSH 2000 kwa masaa 24, cha pili ni cha GB 6 kwa gharama ya TSH 7000 kwa siku 7, na kifurushi cha tatu ni ya GB 16 kwa TSH 20,000 tu kwa siku 30.
Vifurushi hivi maalum na vya gharama nafuu kwa watumiaji wa DStv Now vinapatikana kupitia www.tigosports.co.tz, Tigo Pesa App, na menyu za *147*00# na *148*00#.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Masoko Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo, alisema uzuri wa DStv Mobile app ni kwamba inaweza ikafanya kazi katika vifaa aina nne bila nyongeza ya gharama yeyote.
“Hakutakuwa na gharama ya ziada kutazama DStv kupitia vifaa mbali mbali, kwa sababu gharama zote zinakuwa zimeshalipiwa katika kifurushi cha mwezi cha DStv. Ili kuweza kuangalia mechi za AFCON, wateja wa DStv wanachohitaji kufanya ni kupakua DStv App katika simu janja zao, kompyuta mpakato, tablet au vifaa janja vingine,” alisema Shelukindo.
Uzuri mwingine wa kipekee ambao mteja anaweza kuupata kupitia huduma hii ni kuwa wateja wa DStv wanapewa uwezo wa kuunganisha hadi vifaa vinne tofauti kwa wakati mmoja kutazama vipindi vya DStv wakati huo televisheni nayo ikiwa nayo imeunganishwa na kuendelea kutumika kuangalia vipindi.
Shelukindo aliongeza, “Kujiunga na DStv Now wateja wanatakiwa kutembelea
now.dstv.com, na kufuata maelekezo ya kuweka jina na neno siri. Baada ya kumaliza hatua hiyo rahisi, watakuwa na uwezo wa kupakua na kuingia katika kifaa janja yeyote na taarifa zao walizoweka na kuanza kutazama mubashara vipindi.”
Shelukindo aliongeza kuwa, mechi za AFCON zitakuwa zinaonyeshwa kupitia vifurushi vyote vya DStv kuanzia kifurushi cha bei ya chini kabisa mpaka kifurushi cha DStv Premium. “Wateja wa DStv katika vifurushi vyote watakuwa na uwezo wa kufurahia mechi zote 52 ya mashindano haya maarufu ya mpira. Ushirikiano wetu na Tigo umefanya maisha kuwa rahisi kwa sababu inatoa fursa kwa yeyote kufurahia mechi hizi popote pale,” alisema.