Home Mchanganyiko MAPITIO YA MWONGOZO YAKINIFU WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI YAFANYIKA SERIKALI

MAPITIO YA MWONGOZO YAKINIFU WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI YAFANYIKA SERIKALI

0

Bw. Ronald Komanga Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, akiongelea mafanikio ya Maboresho ya Mwongozo yakinifu wa Kilimo cha umwagiliaji.

Katika Picha Bwana Anthon Nyarubamba ni Meneja Msaidizi wa Mradi wa kujenga uwezo (TANCAID) kutoka Tume a Taifa ya Umwagiliaji akiongea na waandishi wa Habari kuhusu mwongozo wa Umwagiliaji. (Habari na Picha Kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Morogoro)

*****************

Kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa la maendeleo la Japan (JICA)
kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, imefanya mapitio ya mwongozo yakinifu wa
Umwagiliaji unaolenga kufanya mabadiliko na maboresho katika kilimo cha
Umwagiliaji nchini.

Bw. Anthon Nyarubamba ni Meneja Msaidizi wa Mradi wa kujenga uwezo
(TANCAID) kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji amesema hayo leo Mjini
Morogoro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa
kikosi kazi wa kupitia mwongozo huo.

Bw. Nyarubamba alisema kuwa, mwongozo huo ambao ulikuweo tangu mwaka
2010 ambao ulikuwa katika mfumo wa kitabu kikubwa utaboreshwa na kuwekwa
katika lugha rahisi na rafiki kwa watumiaji ambao ni wataalam, wakulima na
wadau wote katika sekta hiyo, ambao utarahisisha na kuonyesha matumizi sahihi
ya maji katika skimu za kilimo cha umwagiliaji.

“Kabla ya kuwepo kwa Mwongozo huu wakulima wengi walikuwa wanadhani
kuwa kilimo cha umwagialiaji ni kilimo chenye kutumia maji mengi lakini
Mwongozo sasa utaonyesha matumizi sahihi ya maji sambamba na kujenga
uwezo kwa wataalam na wakulima nchini.” Alisema Nyarubamba.

Aidha Bwana Nyarumbana aliendelea kusema kuwa, mtu yeyote
atakayeshughulika na kilimo cha umwagiliaji nchini atatakiwa kuufuata mwongozo
huo ambao pia utachangia skimu za kilimo cha umwagiliaji nchini kujengwa katika
ubora.

Awali, Akiongea na waandishi wa Habari baada ya sehemu ya kwanza ya mapitio
ya mwongozo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji kutoka Tume ya Taifa
ya Umwagiliaji Bw. Ronald Komaga amesema tangu kuwepo kwa mwongozo huo
mwaka 2010 kumejitokeza changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na kitabu cha
mwongozo huo kuwa kikubwa na siyo rafiki kwa watumiaji, mwongozo
kutoeleweka kwa wadau wengi na baadhi ya vipengele kutotekelezeka jambo
ambalo limepelekea kuwa na awamu hii ya pili ya mapitio na maboresho ya
mwongozo huo.