Home Michezo MAANDALIZI YA TAIFA STARS-KIKAO NA MH SPIKA

MAANDALIZI YA TAIFA STARS-KIKAO NA MH SPIKA

0

******************

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Job Ndugai,amekutana jana na wachezaji wa timu ya taifa Taifa Stars,katika kambi ya timu hiyo iliyopo nchini Misri.

Katika mazungumzo na wachezaji hao,Mheshimiwa Spika alifikisha ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,John Magufuli,kuwataka vijana hao kupambana kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya taifa katika mashindano ya Afrika yanayotarajia kuanza Juni 21,nchini Misri.

Mheshimiwa Spika,aliwataka wachezaji  hao kuingia uwanjani wakiwa wamejua wamebeba matumaini makubwa kwa Watanzania ambao macho na masikio yao wameyaelekeza kwao.

Kwa upande wa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta,alimuahidi Mheshimiwa Spika kuwa wamepokea salamu za Mheshimiwa Rais,na wamemuahidi kuwa wataingia uwanjani kupambana na kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya taifa.

Alisema,hawataki kumuahidi kitu kikubwa,ila watajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha wanapambana na kupata ushindani katika mechi zote za makundi.