Msemaji Msaidizi Wa Jeshi La Polisi Mrakibu Msaidizi Athuman Mtasha akitoa mada wakati wa warsha ya Taasisi ya Vyombo vya Habari kusini mwa Afrika kwa hapa nchini Tanzania [MISA -TAN] iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa Habari kwa lengo la kuwajengea Uwezo namna ya kuripoti Habari za COVID-19 bila kuleta taharuki katika Jamii.
Mkurugenzi wa MISA-Tan Bw.Gasirigwa Sengiyumva,akiwasilisha maada wakati wa warsha ya Taasisi ya Vyombo vya Habari kusini mwa Afrika kwa hapa nchini Tanzania [MISA -TAN] iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa Habari kwa lengo la kuwajengea Uwezo namna ya kuripoti Habari za COVID-19 bila kuleta taharuki katika Jamii.
…………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Wito huo umetolewa Jijini Dodoma na Msemaji Msaidizi Wa Jeshi La Polisi Mrakibu Msaidizi Athuman Mtasha wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika warsha ya Taasisi ya Vyombo vya Habari kusini mwa Afrika kwa hapa nchini Tanzania [MISA -TAN] iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa Habari kwa lengo la kuwajengea Uwezo namna ya kuripoti Habari za COVID-19 bila kuleta taharuki katika Jamii.
Msemaji msaidizi huyo wa Jeshi la Polisi amesema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakisambaza taarifa za mamlaka mbalimbali zisizo wahusu bila uchunguzi matokeo yake husababisha uchochezi ,takwimu za uongo na kusababisha taharuki katika jamii hivyo ni vyema watu wakaacha mara moja tabia ya kusambaza taarifa kwani zinaweza kuwatia hatiani.
“Kuna mambo haya ya Anti- Propanganda watu wamekuwa wakipost taarifa zisizo wahusu bila takwimu na kusababisha taharuki katika jamii hivyo mtu anapofanya hivyo ni uchochezi na unapotoa taarifa ambayo hauna mamlaka nayo ni kosa hivyo ni wajibu wa kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu na sharia za nchi”amesema.
Afisa sheria Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA]Kanda ya kati Joseph Kavishe amesema mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kushirikiana na vyombo vingine likiwemo Jeshi la polisi imeendelea kusimamia kwa ueledi vyombo vya Habari Pamoja na watumiaji wengine wa mitandao .
“TCRA imeendelea kusimamia kwa ukaribu sana vyombo vya Habari Pamoja na watumiaji wengine wa mitandao, kwa Maagizo ya Mhe.Rais kuhusu taarifa za Uzushi yeyote anayekamatwa lazima taraibu za kisheria kufuatwa ,TCRA inasimamia vyombo vya Habari kwa mashauriano pengine panapokuwa na changamoto Fulani ya utoaji wa Habari huwa kuna kamati ya maudhui na si kila kosa lazima kuadhibiwa na makosa mengine kamati ya maudhui hukaa na kuwaonya wahusika ili kuacha kuleta mkanganyiko katika jamii”amesema.
Mjumbe wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Michael John Gumile ambaye pia ni Mhadhili kutoka chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana[St.John]amesema Warsha hiyo ya wanahabari imesaidia wadau wa Habari namna ya kuandika Habari zitakazosaidia kuondoa taharuki katika jamii hususan katika kipindi hiki cha Corona.
“Sasa hivi nchi na Dunia kwa ujumla hivyo wadau wa Habari tumekutana hapa katika kujenga msingi mzuri ili kuhakikisha taarifa sahihi zinapatikana na watu kuzifanyia maamuzi na taarifa ambazo haziwezi kuleta mkanganyiko katika jamii”amesema.
Meneja wa kituo cha Redio,Dodoma FM ,Zania Miraji ni miongoni mwa wadau wa Habari waliohudhuria katika warsha hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika ,hapa nchini[MISA-TAN]yeye amesema warsha hiyo imekuwa mwarobaini wa kuwakumbusha waliojifunza kutoka vyuoni na na maelekezo yaliyotolewa katika warsha hiyo watayafanyia kazi hususan namna ya kuandika Habari ambazo hazina mkanganyiko pia namna ya mwanahabari ya kujikinga na COVID -19 anapotekeleza majukumu yake ya kila siku.