Home Mchanganyiko NHIF TANGA YAKABIDHI MASHUKA 50 KWA WILAYA YA PANGANI

NHIF TANGA YAKABIDHI MASHUKA 50 KWA WILAYA YA PANGANI

0
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally
Mwakababu kulia akimkabidhi Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif
Ally mashuka yaliyotolewa na mfuko huo kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya
wilaya katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella halfa
hiyo ilifanyika mjini Pangani

 MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally
Mwakababu kulia akimkabidhi Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif
Ally mashuka yaliyotolewa na mfuko huo kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya
wilaya katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella halfa
hiyo ilifanyika mjini Pangan

 MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akizungumza mara baada ya
kukabidhi mashuka hayo katika anayemsikiliza ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Martine Shigella  na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif
Ally

MENEJA
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally
Mwakababu kulia akizungumza mara baada ya kukabidhi mashuka hayo katika
anayesimamia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella 

MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umekabidhi mashuka 50 kwa
ajili ya vituo vya kutoka huduma ya Afya wilayani Pangani ikiwa ni
kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa bora kwa wagonjwa wanapokwenda
kupata matibabu kwenye maeneo hayo

Makabidhiano hayo yalifanywa
na Meneja wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kwa
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif Ally katika halfa
iliyoshuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella.

Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo Meneja Mwakababu alisema wamemkabidhi
Mwenyekiti huyo kwa ajili ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Isaya Mbenje
na vituo vya afya vinavyotoa huduma ya afya wilayani Pangani wakiwa na
dhamira ya bima ya afya ni kuhakikisha huduma zinakuwa bora.

Alisema ili pia lengo kubwa ni kuhakikisha wagonjwa wanapokwenda kupata
huduma wakute mahali safi na salama ambayo yawawawezesha kupata matibabu
kwenye mazingira mazuri yanayovutia.

“Kama mnavyojua NHIF
tunajua Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ni mdau wetu mkubwa na Pangani
ni eneo lake NHIF ikaona tumsapoti kwa upande wa afya kwamba
anapopambana na maji kuhakikisha maji yanapatikana lakini pia
kuhakikisha mazingira ya wananchi kwenye kupata huduma yaweze kuwa
salama”Alisema Meneja huyo.

 Hata
hivyo alisema kwamba wataendelea kushirikiana na wadu wengine katika
kuhakikisha huduma za bima ya afya zinaboreka huku akieleza kwamba
wanataka wananchi wakifika kwenye maeneo ya kupata matibabu waweze kuona
namna yalivyokuwa mazuri na safi wakati wote.