Watanzania wametakiwa kuulinda, kuuenzi na kuuendeleza Muungano kwani ni tunu ya taifa na msingi wa maendeleo ya wananchi wenyewe.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Juma Mohamed Salum leo Novemba 25, 2026 katika mahojiano maalum kwenye kipindi cha Hello Tanzania kinachorushwa na kituo cha Redio cha Uhuru FM.
Alieleza kuwa Muungano umejengeka katika misingi ya umoja, udugu, kuheshimiana na majadiliano kupitia kwa waasisi wake Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.
Dkt. Juma aliwasihi Watanzania kujenga uzalendo na kuchukua katika kuhakikisha Muungano huu adhimu unalindwa ili uendelee kuwanufasha kupitia fursa mbalimbali zinazopatikana.
Alisema kuwa zipo fursa mbalimbali zinazopatikana kutoka pande zote mbili za Muungano yaani Tanzania Bara na Zanzibar zikiwemo za kijamii na kiuchumi hususan biashara ambazo zimekuwa zikiwanufaisha wananchi.
“Muungano una manufaa makubwa kwa wananchi wa pande zote mbili ni kawaida kukuta mwananchi kutoka Zanzibar akifanya biashara upande wa Tanzania Bara na mwananchi kutoka upande wa Zanzibar akifanya biashara Bara na katika kijamii leo hii Mnyamwezi ameoa Zanziba yote hayo ni matunda ya Muungano,” alisema.
Akiendelea kuzungumza katika kipindi hicho, Mkurugenzi huyo alieleza kuwa Muungano huu ni imara, madhubuti na wa kipekee barani Afrika na duniani kwa ujumla.
Alisema Muungano huu ulioasisiwa Aprili 26, 2964 ukiwa tayari umetimiza miaka 62 umeendelea kudumu na hivyo kuwa wa mfano wa kuigwa na barani Afrika na duniani kwa ujumla.
Hivyo, wananchi wanapaswa kuonesha uzalendo kwa vitendo wakati wa Serikali zote mbili zikiendelea kushirikiana ili kudumisha Muungano huu kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
