Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 18 Novemba, 2026 anaondoka nchini kwenda nchini Uganda kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa ya siku mbili, kwa mwaliko wa Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda.

Akiwa nchini Uganda, Rais Dkt. Samia atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais Museveni, yatakayooangazia kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Uganda katika sekta za nishati, kilimo, viwanda, biashara na fedha.

Aidha, kwa kushirikiana na Rais mwenyekiti, atatembelea na kuzindua kiwanda cha kuunganisha magari cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Wilaya ya Mpigi, nchini humo.

Ziara ya Rais Dkt. Samia inalenga kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda na kupanua fursa za kiuchumi kwa manufaa kwa wananchi wa pande zote mbili.