Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mtendaji wa Programu wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dkt. Khamis Khalid Said, wakati wa kufungua rasmi Kikao cha Kitaalamu cha Kuhakiki Rasimu ya Mpango Mkuu wa Usimamizi (GMP) wa Hifadhi ya Biosphere ya RUMAKI kilichofanyika katika Ukumbi wa TUJIWAKI, Kilwa Masoko, Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi.
Kikao hiki kinalenga kupitia na kuboresha rasimu ya mpango huo ili kuhakikisha unazingatia changamoto zinazokabili mifumo ikolojia ya bahari na pwani, zikiwemo athari za mabadiliko ya tabianchi, uvuvi uliokithiri na uharibifu wa makazi ya viumbe vya baharini.
Mpango huo unalenga kulinda mifumo muhimu ya ikolojia, ikiwemo misitu ya mikoko, miamba ya matumbawe na maeneo ya kutagia mayai ya kasa, sambamba na kuimarisha maisha ya jamii za pwani kupitia uvuvi endelevu, utalii wa kiikolojia na ufugaji endelevu wa viumbe vya majini.



