Wajasiriamali wadogo na wakati wakifuatilia maelekezo kutoka kwa mwezeshaji (hayupo pichani) wakati wa mafunzo ya namna ya kuboresha biashara zao pamoja na kufahamu mbinu za kujua masoko, bidhaa na namna ya kuuza na kupata faida. Mafunzo hayo yametolewa na Kituo cha Ubunifu na Ujasiriamali cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDIEC) kwa kushirikiana na ufadhili wa European Investment Bank (EIB) katika jengo la Shule kuu ya Biashara kuanzia tarehe 13 hadi 15 Mei, 2019.
Wajasiriamali wadogo na Wakati wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Ujasiriamali yaliyoendeshwa na Kituo cha Ubunifu na Ujasiriamali cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDIEC) kwa kushirikiana na ufadhili wa European Investment Bank (EIB) katika Jengo la Shule kuu ya Biashara chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Mteja kutoka Benki ya Access Alexander akiwaeleza wajasiriamali wadogo na wakati huduma zinazotolewa na benki ya Access, na namna bora ya kutunza fedha katika akaunti tofauti zilizopo katika benki hiyo pamoja na kuwafundisha mbinu za kuwekeza na kukuza mitaji ili waweze kukopesheka kwa urahisi.
NA EMMANUEL MBATILO
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Shule Kuu ya Biashara (UBDS),kupitia Kituo cha Ubunifu na Ujasiriamali cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDIEC) kwa kushirikiana na ufadhili wa European Investment Bank (EIB) kimetoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo na wakati juu ya ufahamu kwenye biashara na mipango kabla ya kuanza biashara.
Miongoni mwa masuala waliyofundishwa ni pamoja na kujua mipango ya kibiashara, vyanzo vya fedha, kujua masoko, namna ya kuwa na bidhaa bora na jinsi ya kuuza kwa faida pamoja na kufundishwa namna bora ya
kuandaa maandiko ya kibiashara.
Mafunzo hayo ya siku tatu yalianza tarehe 13 na kumalizika Tarehe 15 Mei 2019 yameshirikisha wajasiriamali kutoka ndani na nje ya Dar es Salaam ili kuweza kutoa nafasi na wigo mpana kwa wajasirimali kujikumbusha mbinu na namna bora za kuboresha biashara zao.