Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akitoa maelekezo kwa Viongozi na wasimamizi wa ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo iliyopo katika Kijiji cha Kiamili, akiwa ziarani mkoani Ruvuma, leo tarehe 10 Novemba 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, akiwa ziarani mkoani Ruvuma, leo tarehe 09 Novemba 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi wanaopata huduma katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, wakati alipotembelea hospitali hiyo, akiwa ziarani mkoani Ruvuma, leo tarehe 10 Novemba 2026.
Muonekano wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, iliyokaguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa ziarani mkoani Ruvuma, leo tarehe 10 Novemba 2026.
……………
Makamu wa Rais, Mhe. Deogratius Ndejembi, amekagua ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mbinga wenye thamani ya Shilingi bilioni 3.7, ambapo majengo 15 kati ya 29 yamekamilika tangu mradi huo uanze mwaka 2021.
Katika ziara hiyo, ameuagiza uongozi wa Halmashauri kutumia sehemu ya mapato yake ya ndani, yanayofikia wastani wa Shilingi bilioni 14.7 kwa mwaka, kuharakisha ukamilishaji wa baadhi ya majengo hasa nyumba za wafanyakazi badala ya kutegemea fedha za Serikali Kuu pekee.
Aidha, amepongeza mafanikio katika kuboresha huduma za uzazi na kupunguza vifo vya mama na mtoto vilivyoripotiwa hospitalini hapo kutoka 550 Kabla ya ujenzi wa hospitali hiyo hadi 106 tangu hospitali ilipoanza kutoa huduma. Akieleza sababu za idadi ya Vifo, Mganga Mkuu katika hospitali hiyo amesema idadi kubwa ya Vifo inatokana na wajawazito kujifungulia nyumbani.
Akifikisha salamu za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wagonjwa, Makamu wa Rais amesisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kuimarisha miundombinu na huduma za afya ili kulinda maisha ya mama na mtoto.

