Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema amani na utulivu ni msingi wa maendeleo ya nchi, hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kuvilinda ili kuendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji, biashara, utalii na shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii.
Alhaj Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 09 Novemba 2026, katika Dua Maalumu ya Kitaifa ya kuiombea nchi amani na ulinzi dhidi ya majanga mbalimbali, iliyofanyika Msikiti wa Muembe Shauri, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Dkt. Mwinyi amesema Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 ulifanyika katika mazingira ya amani, na amevipongeza CCM na ACT-Wazalendo kwa maridhiano yaliyowezesha kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa kuzingatia maslahi ya Zanzibar na wananchi wake.
Pia amewataka viongozi wa dini kuendelea kuwahimiza waumini kudumisha umoja, mshikamano na kuheshimiana, pamoja na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani na utulivu.
Akizungumzia mvua za Vuli, Alhaj Dkt. Mwinyi amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na El NiƱo, hususan wanaoishi maeneo hatarishi, huku akisisitiza usafishaji wa mitaro na njia za maji pamoja na kuzingatia maelekezo ya Serikali.
Amesema maombi kwa Mwenyezi Mungu yanapaswa kwenda sambamba na hatua za kujikinga dhidi ya majanga.
Dua hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.

