Waziri Mkuu wa DRC atua Tanzania
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Judith Suminwa Tuluka amewasili nchini Tanzania tayari kushiriki Mkutano wa Kwanza wa Wanawake Wabunge wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (Women’s Parliamentary Conference – WPC 2026).
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Tuluka amepokelewa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki
Mhe. Tuluka ni Mgeni Maalum katika mkutano huo unaoanza Novemba 2 hadi 5, 2026 katika ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam.

