Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mpango wa kuzuia uingizaji wa bidhaa chakavu za umeme (used) kutoka nje ya nchi ili kuhifadhi mazingira na kulinda afya za wananchi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Bishara na Maendeleo ya Viwanda Mhe Dkt Salum Soud Hamed katika Mkutano na wafanyabiashara wa bidhaa chakavu za umeme wakati akitoa taarifa ya Serikali kwa bidhaa hizo ambazo zimetumika, katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Wilaya ya Mjini
Amesema Serikali inatarajia kufungia bidhaa hizo baada ya kipindi cha miezi 12 ili kutoa muda kwa wafanyabiasha kuuza bidha zilipo na kupunguza hasara kwa jamii.
Naibu huyo amezitaja bidhaa zitakazofungiwa ni pamoja na komputa na friji ili kupunguza uharibifu wa mazingira na kulinda afya za wananchi.
“Kila biashara lazima iwekewe taratibu zake na hii biashara ya vitu chakavu vya umeme lazima nayo iwekewe taratibu zake” amesema Mhe Dkt Salum
Ameeleza kuwa bidhaa nyingi zinazoingizwa nchini hazifai na zinakuwa hatarishi kwa mtumiaji pia huchafua mazingira kwa ujumla pamoja na kusababisha maradhi mbalimbali jambo ambalo linarudisha nyumba maendeleo ya wananchi
Amesema kuwa kuwekwa kwa taratibu hizo si kumkandamiza mfanya biashara bali serikali inakusudi kumlinda mtumiaji na maslahi ya taifa kwa ujumla.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Habiba Hassan Omar amesema Serikali imeamua kuweka utaratibu huo kwa kushirikiana na wafanyabiashara pamoja na wadau mbalimbali wa biashara na kuangalia athari ambazo zinazojitokeza kutokana na bidhaa hizo.
Aidha amefahamisha kuwa kutokana na changamoto hizo Serikali kwa kushirikiana na wadau wa bishara imekuwa na mpango wa kuzuia uingizaji wa bidhaa hizo kwa maslahi wa wananch na Taifa kwa ujumla.
Nao wafanyabiashara wameomba kuwekewa vikao ili kupata muda wa kutafakari hatua zinazoweza kufanyika ili kuepuka hasara katika biashara hiyo

