Kampuni ya mawasiliano ya Yas imeungana na washiriki wengine katika mbio za kwanza za Tanzania-China Nyerere Run 2026 kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mbio hizo zilifanyika Oktoba 14, zikianzia na kuishia katika kituo cha EACLC, Ubungo jijini Dar es Salaam. Mbali na kumuenzi Mwalimu Nyerere, mbio hizo zililenga kuhamasisha mazoezi kwa afya bora na kusherehekea urafiki wa kihistoria kati ya Tanzania na China.

YAS YASHIRIKI TANZANIA-CHINA NYERERE RUN KUMUENZI BABA WA TAIFA
