CHIRWA
Ramadhani Singano
Joseph Kimwaga
****************************
NA EMMANUEL MBATILO
Uongozi wa klabu ya Azam FC umetangaza idadi ya wachezaji ambao hawatendelea kuwa nao katika kikosi chao msimu ujao wa ligi pamoja na michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.
Wachezaji wa kigeni ambao wameonyeshwa mlango wa kutokea ni Obrey Chirwa, Enock Atta Agyei na Steven Kingue
Kwa upande wa wachezaji wa nyumbani waliotemwa ni, Ramadhani Singano, Joseph Kimwaga, Hassan Mwasapili na Danny Lyanga.
Licha ya viwanga walivyovionyesha kuisaidia klabu hiyo kunyakua taji la FA lakini klabu hiyo haikushawishika kubaki nao wachezaji hao hivyo wameamua kuwaachia ili wakajaribu bahati yao katika klabu nyingine