Sumbawanga
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hamida Khamis ameipongeza TARURA kwa juhudi za kuimarisha miundombinu ya barabara, hususan maeneo ya vijijini, zinazochochea shughuli za kiuchumi na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa wananchi.
Mhe. Hamida ameyasema hayo alipotembelea banda la TARURA katika Maonesho ya Vijana yanayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ndua mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
Aidha, ameutaka Wakala huo usiache kubadilishana ujuzi na wataalam kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hususan kwenye ujenzi wa madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe ambayo hutumia malighafi inayopatikana kwenye eneo linalotekelezwa mradi husika.

