Mkuu wa idara ya mauzo kwa biashara ndogo na za kati Jasmine Makori (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Pius Maswaga wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zawadi ikiwa ni ishara ya shukrani kwa ushirikiano, wakati wa ziara ya Vodacom Business kwa wateja wao, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Mkuu wa idara ya Huduma kwa Wateja Deogratius Massawe (kushoto) akimkabidhi Afisa Mtendaji Mkuu wa Green Telecom Bw Rahul Sahni zawadi ikiwa ni ishara ya shukrani kwa ushirikiano wao, wakati wa ziara ya Vodacom Business kwa wateja wao, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

 Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (kulia) akimkabidhi mwakilishi wa Access Bank zawadi kama ishara ya shukrani kwa ushirikiano wao, wakati wa ziara ya Vodacom Business kwa wateja wao, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.Mawakala walioshiriki katika mafunzo yaliyoandaliwa na Vodacom Business kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu bidhaa na huduma zinazotolewa na idara hiyo, ili kuwawezesha kuzifahamu na kuwahudumia wateja kwa ufanisi zaidi, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo hayo, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.