
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Mhandisi Nickson Babu (kulia), akimkabidhi Hussein Mchomvu wa Idara ya Ufundi zawadi ya pongezi kwa kutambua mchango wake kazini, wakati wa hafla ya kufunga Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026, iliyofanyika Oktoba 9 katika ofisi za shirika hilo, Kurasini, Dar es Salaam.

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya Yombo (kushoto) Mhandisi Elirehema Makacha akimkabidhi Angela Kalambo wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja, Ofisi ya Wilaya ya Yombo zawadi ya pongezi kwa kutambua mchango wake kazini, wakati wa hafla ya kufunga Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026

Mtumishi Bora TANESCO Wilaya ya Mbagala kutoka Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja, Mustapha Hamza, akishika cheti cha pongezi alichotunukiwa kwa kutambua utendaji wake bora kazini.


Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Mhandisi Nickson Babu akizungumza na wafanyakazi wa mkoa huo wakati akifunga Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026

Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa wa Temeke, Lucia Renatus akitoa taarifa namna mkoa huo ulivyoshiriki Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026


Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Mhandisi Nickson Babu, akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo wakikata keki katika hafla ya kuhitimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026


Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Temeke wakiwa katika hafla ya kuhitimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026
…………..
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Tememe limetoa Tuzo kwa watumishi wake waliofanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa wafanyakazi.
Akizungumza leo, Oktoba 9, 2026, wakati wa hafla ya kufunga Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 iliyofanika ofisi za TANESCO Mkoa wa Temeke, Kurasini, Dar es Salaam,
Meneja wa mkoa huo, Mhandisi Nickson Babu, amewataka watumishi kutekeleza majukumu kwa uzalendo na kujituma zaidi ya wajibu wao wa kawaida ili kuongeza ufanisi na kutoa huduma bora.
Mhandisi Babu, amesisitiza umuhimu wa nidhamu, uwajibikaji na kujituma kazini kwa watumishi ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja.
Katika hafla hiyo, uongozi wa TANESCO Mkoa wa Temeke umetambua mchango wa watumishi waliofanya vizuri katika maeneo yao ya kazi, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha uwajibikaji na kuimarisha utendaji ya shirika hilo.
Wafanyakazi waliotambuliwa kuwa kinara katika maeneo ya kazi ni Hussein Mchomvu kutoka Idara ya Ufundi, Ofisi ya Mkoa wa Temeke; Mustapha Hamza kutoka Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja, Ofisi ya Wilaya ya Mbagala;
Mwengine ni Angela Kalambo kutoka Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja, Ofisi ya Wilaya ya Yombo.
Wakizungumza kwa niaba ya wenzao, wafanyakazi hao wameushukuru uongozi kwa kutambua mchango wao, wakieleza kuwa hatua hiyo ni chachu ya kuongeza juhudi na kuendelea kutekeleza majukumu kwa ufanisi.
Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 yenye kaulimbiu isemayo “Mbele Zaidi Kihuduma,” TANESCO Mkoa wa Temeke ilifanya shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya usafi wa mazingira, kufanya Kikao kazi na wadau wa nishati,
pamoja na vikao vya watumishi vilivyolenga kuweka mikakati ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja
