Na Victor Masangu, Pwani
Waziri wa  afya Mohamed  Mchengerwa  katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita  Dkt. Samia Suluhu Hassaan katika kuwakomboa wanawake na kuimarisha jumuiya zao  amemua kuchangia kiasi cha shilingi milioni 35 kwa ajili ya kuwasaidia umoja wa wanawake wa (UWT) Mkoa wa Pwani waweze kukamilisha malengo yao waliyojiwekea ikiwemo suala la ujenzi  wa nyumba za makatibu wa Wilaya na ngazi ya Mkoa.
Mchengerwa ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi  (MNEC )  Taifa ameyabainisha  hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika  kikao cha baraza la kawaida la uwt Mkoa wa Pwani ambalo limehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama pamoja na viongozi wa serikali akiwemo Mkuu mpya  wa Mkoa wa  Pwani.
 
Mchengrwa amebainisha  kwamba lengo lake kubwa ni kuendelea kutoa sapoti kwa kuweza kuwasaidia kwa hali na mali wanawake wa jumuiya hiyo ya UWT ikiwemo kuwapatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya nyumba za makatibu kuanzia ngazi ya Mkoa pamoja na ngazi za Wilaya.
“Nimefarijika  sana kualikwa katika kikao hiki cha baraza la kawaida la UWT Mkoa wa Pwani na nimechangia kiasi cha shilingi milioni 35 na laki moja  kwa ajili ya kuwasaidia wanawake hao katika mambo mbali mbali ikiwemo  miradi ya ujenzi wa nyumba za makatibu wa UWT ngazi za Wilaya na ngazi ya  Mkoa na mimi nitapenda sana kuona wanawake mnajikomboa kiuchumi,”amebainisha Waziri Mchengerwa.
Aidha Mchengerwa amewahimiza wanawake wa Mkoa wa  Pwani kuachana na tabia ya kuwa wanafiki na badala  yake amewataka  kuhakikisha kwamba wanaweka misingi imara ya kutunza amani ya nchi ikiwa sambamba na kushikamana  kwa pamoja kwa  lengo la kuweza kuimarisha jumuiya yao   pamoja na  chama kwa ujumla.
Naye  Mbunge  wa viti maalumu Mkoa wa Pwani Mhe. Mariam Ibrahimu  katika kuwakomboa wanawake hao kiuchumi ametoa pikipiki  zipatazo kumi  kwa ajili ya kuendeshea kama mradi  ambazo  kati ya hizo nane zitakwenda kusaidia   katika ngazi za  Wilaya zote za  UWT  pamoja na nyiingine mbili zitakwenda katika ofisi na UWT  Mkoa  na nyingine ofsikwa wilaya zote za Mkoa wa Pwani  

“Nimeamua kutumia  fedha zangu za mshahara  kwa ajili ya kusaidia  wanawake  wa Mkoa wa Pwani ambapo nimekabidhi pikipiki  kumi ambazo zitasaidia jumuiya za wanawake katika Wilaya zote na kwamba ni mradi ambazo  utaweza  kuwakomboa  katika kujikwamua kiuchumi na kuachana na kuwa  tegemezi na vifaa  vya ujenzi wa nyumba   vyenye thamani ya shilingi  milioni 20  ,”amebainisha Mh.Mariam 

Kwa upande  wake Mwenyekiti  wa  UWT  Mkoa  wa  Pwani  Zainabu  Vullu  amesema  kwamba mikakati  ambayo wamejiwekea ni kuondokana na kuwa tegemezi na kwamba lengo kubwa  ni  kuwa na miradi mbali mbali ya  maendeleo ambayo  itakuwa na tija zaidi katika kuwasaidia wanawake.

Naye Katibu wa UWT Mkoa wa Pwani  Aziza  Omary  amesema  kwamba kwa sasa wamejipanga na kuweka mipango madhubuti ya kuwa na miradi mbali mbali ikiwemo kuwepo na miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa  nyumba za makatibu kwa ngazi ya Wilaya na ngazi ya Mkoa.

Akitoa salama za serikali Mkuu wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo  amewahimiza wanawake  fursa  za  asilimia 10  ambazo  zinatengwa na   Halmashauri  kwa lengo la kuweza  kuwasaidia sana  wanawake katika kujikwamua kiuchumi.

Katika  kikao cha baraza la  UWT   Mkoa wa Pwani wameweza kujadili mambo mb  ali mbali yakiwemo suala uanzishwaji wa  miradi ya maendeleo ili kujikwamua kiuchumi, ujenzi wa nyumba za makatibu wa Wilaya pamoja na Mkoa,mikakati ya kuimarisha jumuiya  na uhai wa wanachama,  pamoja jinsi watakavyoweza kutimia fursa za mradi wa pikipiki  ambazo wamepatiwa kama ni moja ya kitega uchumi.