Wajumbe wa CCM Wilaya ya Chamwino wamemaliza kupiga kura za maoni kuwatafuta watakaowania nafasi ya ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chamwino, huku ushindani mkubwa ukionekana kati ya Dkt. Netho Ndilito na Dkt. Kedmon Mapana.

Matokeo ya jumla yanaonesha Dkt. Ndilito akiibuka na kura 2,401, akifuatiwa na Dkt. Mapana aliyepata kura 1,927, tofauti ya kura 474.

Hata hivyo, swali linalobaki ni je, vikao vya CCM vitamteua nani kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi huo mdogo kati ya watia nia wote 34?

Uchaguzi huo unafuatia nafasi kuachwa wazi na Mhe. Deogratius Ndejembi, aliyeteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.