Kuna picha unayoitazama kwa sekunde chache tu, lakini moyo wako unaendelea kuizungumza kwa muda mrefu.

Hii ni picha yangu bora zaidi kwa miaka yote, si kwa sababu ya uzuri wake, bali kwa sababu ya somo kubwa lililofichika ndani yake.

Sisi binaadamu mara nyingi tunaamini kwamba mtu mwenye hali ya chini ndiye anayepaswa kupewa na yule mwenye nacho. Lakini watoto hawa wametufundisha somo tofauti kabisa.

Mmoja alianza kutoa Shilingi mia moja ya hela yake ya break na kumpa Mhe. Rais. Mwingine akafuata. Mwisho wa yote, Mhe. Rais akajikuta ameondoka na Shilingi 2,800 ambazo watoto hawa walitoa kutoka katika kile kidogo walichokuwa nacho mifukoni.

Hawakuwa na vingi, lakini walitoa kwa moyo.

Wakati mwingine tunasahau kwamba thamani ya kutoa haipimwi kwa kiasi unachotoa, bali kwa moyo uliokusukuma kutoa.

Watoto hawa wametukumbusha jambo moja kubwa: wengi wetu tumezoea kufikiria kuhusu kupokea, lakini si mara zote tunakumbuka kutoa.

Picha hii ibaki kuwa ukumbusho kwamba hata kile kidogo ulicho nacho kinaweza kuwa kikubwa sana kwa mwingine.

Kuwa sababu ya tabasamu la mtu leo.