Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Baraza la Famasi limeadhimisha Siku ya Wafamasia Duniani leo Septemba 25, 2026 kwa kufanya shughuli za kijamii (CSR) kwa kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa wahitaji na wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (RRH) na Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Tumaini Foundation, kilichopo Ihumwa.
Baraza hilo limeeleza kuwa zoezi hilo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira yake ya kurejesha fadhila kwa jamii, kuimarisha mshikamano na kudhihirisha kuwa taaluma ya famasi ina nafasi muhimu katika kuchangia ustawi na afya ya jamii.
Katika maadhimisho hayo, Baraza la Famasi limewatakia wafamasia wote nchini na duniani kote maadhimisho mema ya Siku ya Wafamasia Duniani, huku likisisitiza umuhimu wa taaluma hiyo katika kuhudumia jamii na kuboresha afya za wananchi.

