Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Kisheria ya Mkoa wa Singida, ambaye ni Wakili wa Serikali Mkoa wa Singida, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, *Bi. Matrider Meckson* ameiongoza kamati hiyo katika kutoa huduma za ushauri wa kisheria bila malipo kwa wananchi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Singida, huduma hizo zimeanza kutolewa kuanzia tarehe 24 kuendelea hadi tarehe 30 Septemba, 2026.

Kamati hiyo imeendelea na utaratibu wa kutoa huduma za ushauri wa kisheria kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa mkoa huo, ambapo huduma hiyo inatolewa bure na jopo la Mawakili wa Serikali.

Kutolewa kwa huduma hizo ni mwendelezo na mkakati wa Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa kusogeza huduma za kisheria karibu zaidi na wananchi, kutatua changamoto za kisheria zikiwa katika hatua za awali (Preventive Legal Care) pamoja na kuendelea kurejesha tabasamu kwa Wananchi.