Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu Aggrey Mwanri, amewasili katika Ofisi za CCM Wilaya ya Same kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi katika wilaya hiyo.

Katika ziara hiyo, Mwanri anatarajiwa kutembelea Majimbo ya Same Mashariki na Same Magharibi, ambako atakutana na viongozi, wanachama na wananchi katika maeneo mbalimbali.

Ziara hiyo inatarajiwa kuhitimishwa kwa mkutano wa hadhara, ambapo Mwanri atazungumza na wananchi pamoja na wanachama wa CCM wa Wilaya ya Same kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu chama na maendeleo ya jamii.