Na. Meleka Kulwa – Fullshangwe Blog, Dodoma
Ufaulu wa mitihani ya kitaaluma ya Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) umeongezeka kutoka wastani wa asilimia 49.3 katika mitihani iliyopita hadi asilimia 52.1 katika mitihani iliyofanyika Agosti 31 hadi Septemba 4, 2026.
Akizungumza na waandishi wa habari Septemba 18, 2026 jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, CPSP Godfred Mbanyi, amesema watahiniwa 275 kati ya 528 waliofanya mitihani hiyo wamefaulu, sawa na asilimia 52.1.
Amesema jumla ya watahiniwa 567 walijipanga kufanya mitihani hiyo, ambapo 528 walifanya huku 39 wakishindwa kufika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo za kikazi na kiafya.
Aidha, amebainisha kuwa watahiniwa 232, sawa na asilimia 43.9, wamefaulu baadhi ya masomo na kubakiwa na masomo ya kurudia, huku watahiniwa 21, sawa na asilimia 4.1, wakifeli katika hatua zote za mitihani walizofanya na hivyo kutakiwa kurudia examination block nzima.
Amesema watahiniwa wenye masomo ya kurudia watapata fursa ya kufanya mitihani hiyo Novemba 9 hadi 13, 2026, huku dirisha la usajili likiwa limefunguliwa baada ya kikao cha Bodi.
Pia, ameongeza kuwa watahiniwa wenye last chance referrals wanapaswa kutumia nafasi ya mitihani ya Novemba, akieleza kuwa mtahiniwa anayefeli hupewa mikao mitatu mfululizo ya kufanya mtihani kabla ya referral status yake kufutwa na kutakiwa kurudia block nzima.
Aidha, amewataka watahiniwa kuzingatia kanuni na taratibu za mitihani, akisema Bodi haitasita kuchukua hatua kali dhidi ya watakaobainika kufanya udanganyifu, ikiwemo kufutiwa matokeo na kusimamishwa kufanya mitihani kwa mikao mitatu mfululizo.
Amebainisha kuwa kulingana na mazingira ya udanganyifu, mtahiniwa anaweza pia kufikishwa mahakamani, huku taarifa za mtahiniwa aliyeajiriwa zikiwasilishwa kwa mwajiri wake na ambaye hajaajiriwa taarifa zake kuwasilishwa Sekretarieti ya Ajira.
Pia amewakaribisha wahitimu wa vyuo vikuu nchini na wale waliosoma nje ya nchi na kuthibitishwa na TCU au NACTVET kujisajili kufanya mitihani ya kitaaluma ya PSPTB kulingana na sifa walizonazo, huku wazazi, wadhamini na waajiri wakihimizwa kuwasaidia watahiniwa kugharamia maandalizi na ada za mitihani.
Ameongeza kuwa watahiniwa wenye masomo ya kurudia watapata fursa ya kufanya mitihani hiyo Novemba 9 hadi 13, 2026, huku dirisha la usajili likiwa limefunguliwa baada ya kikao cha Bodi.
Aidha ,amewataka watahiniwa wenye last chance referrals kutumia vema nafasi ya mitihani ya Novemba, akieleza kuwa mtahiniwa anayefeli hupewa nafasi tatu mfululizo za kufanya mtihani kabla ya referral status yake kufutwa na kulazimika kurudia block nzima.
Pia, ameongeza kuwa PSPTB itafanya mahafali ya 15 Oktoba 23, 2026 katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam, ambapo wahitimu waliofaulu mitihani yote ya Diploma 1 na 2, Graduate Professional 1, 2 na 3 pamoja na waliofaulu utafiti watatunukiwa vyeti kulingana na ngazi zao, ikiwemo CPSP.
( PICHA ZOTE NA FULLSHANGWE BLOG )
