Na Sixmund Begashe, Dodoma

TIMU za Kamba Wanaume (ME) na Wanawake (KE), Wizara ya Maliasili na Utalii zimewapa somo timu za Wizara ya Kilimo Kamba ME na KE kwa ushindi wa 2-0.

Katika michezo hiyo ya kirafiki, timu za wanaume zilianza kutoana jasho na Maliasili kuibuka na ushindi wa 2-0 na kisha timu za wanawake zikafuatia na matokeo yakawa Maliasili kushinda 2-0.

Baada ya michezo ya awali kumalizika, katika hali isiyo ya kawaida timu ya Kilimo ME, wakaomba kujiuliza tena kwa Maliasili ambapo kwenye mchuano huo timu zote zilitoshana nguvu.

Timu hizo zote zipo kwenye maandalizi makali tayari kwa michuoano ya SHIMIWI 2026 itakayorindima Moshi Mkoani Kilimanjaro hivi karibuni.